TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, April 17, 2014

WATAMBUE MASTAA 10 WENYE NGUVU YA MASHABIKI TANZANIA WEMA BADO HANA MPINZANI ANGALIA HAPA..!


Wakati mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni wazo mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na ugunduzi gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio mastaa 20 wa burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa zaidi 1. Wema Sepetu Well, well, well kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini mrembo huyu akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini ukiugeuza umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara na jinsi anavyokubalika, hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand inayouzika kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti ya udaku ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa Tanzania. Iwe picha akiwa kwa daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa nywele, tattoo aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha zinamuonesha akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu Wema kinavutia attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata comments nyingi kuliko za wengine wote. Kama leo hii Wema akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana, haitachukua muda kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper! Kama akiingia ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda kutokana na watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati akielekea sehemu ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa muigizaji wa orodha A Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame Films, Wema Sepetu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa. Ni msanii gani Tanzania ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata kupigwa redioni? Bila shaka umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani siku za hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la wanyonge walio kwenye mahaba mazito. Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote zimekuwa zikitumiwa na watu wa rika mbalimbali, madaraja tofauti ya kiuchumi, wanawake kwa wanaume na watoto kama burudisho la roho zao. Diamond Platnumz hi hitmaker na haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya Tanzania na kwa kulipwa gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda huu. Hujaza kumbi kubwa za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii mwingine na kuwaacha wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na kutamani walau kukishika tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa mazoezi. Kwa mujibu wa kampuni ya Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT). Pamoja na kuzungukwa na scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana mwenye mawazo pevu na ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni na kupata misukosuko mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa zaidi na mama yake, Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo watafutaji wa maisha wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana wenzie kuhusiana na umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu mwenyezi Mungu na kutokata tamaa. Katika kuhakikisha kuwa anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza kuwa na nia ya kujenga msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na ushawishi?
Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP. Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 90,000. Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
Nancy Sumari ni msichana mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania wa kwanza aliyewahi kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World ambapo mwaka 2005 alifanikiwa kuwa Miss World Africa. Kwa sasa Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia ni mjasiriamali na anafanya kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha watoto wa kike kujitambua na kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao. Katika harakati zake za kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua haki zao, anaendesha programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka kwenye shule mbalimbali za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza nao kuhusu maisha. “Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na wanafunzi na wao wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana mawazo jinsi ya kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza kufanikiwa, na wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari Leo hivi karibuni. Pamoja na hayo pia Nancy anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwenye kampeni ya kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za sekondari za serikali nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu. Hivi karibuni alizindua kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’ kinachomlenga mtoto wa kike kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa licha ya kupitia changamoto mbalimbali. “Ninaamini kitabu kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu niufikishe kwa njia hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga kitu kwenye akili ya mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao watathubutu” aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa kutoka kwa mrembo huyu

No comments:

Post a Comment