Mafundi toka Ujerumani wakiwa kwenye hatua za mwisho kufunga mitambo hiyo hivi karibuni
Naibu Waziri wa Mawasiliano Mh January Makamba akiwa na Mh Hemed Shabiby Mbunge wa Gairo ambao waheshimiwa hao wamepongeza ujio wa radio hiyo mpya inasubiliwa kwa hamu kubwa na wananchi.
Vifaa vya ndani radio hiyo ya kisasa itakayokuwa inapatikana masafa ya 93.7 fm.
Chumba cha ON AIR CHA 93.7 FM kama kinavyooneka kwa ndani.
Na Livingstone Mkoi
Kituo kipya cha radio kitakachopatikana masafa ya 93.7 Fm Jijini Dar siku zake zinahesabika kuanzia sasa kabla ya kuwafikia wananchi wote Tanzania.
Kwa mujibu wa mmoja wa wakurugenzi wa kituo hicho aliiambia Xdeejayz kuwa" Aah tunamshukuru Mungu sehemu kubwa ya maandalizi ni kama imeisha na tuko kwenye hatua za mwisho kuiachia hewani ili mashabiki wapate kile kilichokuwa kimekosekana kwenye radio hizi nyingine" Alisema Mkurugenzi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa madai kuwa bado ni mapema sana.
Aidha kigogo huyo aliongeza kusema kuwa watafanya uzinduzi kwa mashabiki ili kuwatendea haki" Unajua mshabiki ndiyo wasikilizaji hivyo ni vyema tukawapa kipaumbele wao na sio siku nyingi tutafanya uzinduzi rasmi ili wapate nafasi ya kuwa karibu na radio yao" Alisema
Katika hatua nyingine mwishoni mwa juma waheshimiwa wabunge Jijini Dodoma walipongeza ujio wa radio hiyo mpya ikayoanza kupatikana zaidi ya mikoa sita kutokana na mitambo yao kuwa ya kisasa na yenye nguvu kubwa.
No comments:
Post a Comment