TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, March 31, 2014

WAHESHIMIWA WABUNGE HAWA WAIZUNGUMZIA RADIO MPYA 93.7 FM DAR ES SALAAM, WATOA PONGEZI KWA TCRA KWA KUTOA KIBARI HICHO WAWAASA VIJANA WENYE VIOPAJI VYA MUZIKI KUCHANGAMKIA HARAKA!





Na Livingstone Mkoi aliyeko Dodoma
Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hatimae wamefunguka na kuizungumzia ujio mpya wa kituo cha radio mpya itakayopatikana kwa masafa ya 93.7 Fm Dar es Salaam.
Mwwandishi wa Blog hii ambae yuko Mkoani Dodoma kimajukumu ya kiofisi alifanikiwa kuzungumza na baadhi ya waheshiwa wabunge hao vijana ambao ni vipenzi vya watu nchini na kwenye majimbo yao ambapo mtu wa kwanza kuzungumza alikuwa Mbunge Gairo Mh Hemed Shabiby alisema" Tunawapongeza sana wamiliki wa radio hiyo mpya kwani itasaidia kuwainua vijana wengi na kwani ifahamike kuwa muziki ni ajira kama ilivyo kwa ajira nyingine hivyo pongezi kwa wamiliki wa kituo hicho" Alisema Mh huyo 

Aidha nae Mbunge wa Kawe Jijini Dar Halima Mdee alipongeza ongezeko la medio nchini kwani utaleta mafanikio yaa nchi " Hiyo ni nzuri kwa kweli nami pia naungana na waheshimiwa wengine kuwapa hongera wamiliki wa kituo hicho kwani kwa sasa vijana wengi wanatamani kuimba hata kule kwenye jimbo langu kuna wanamuziki wengi sana wachanga ambao kufunguliwa kwa radio hiyo kutasaidia kuwatambulisha" Alisema Mh Mdee ambae ni kipenzi cha wananchi wa Kawe
Hata hivyo nae Mh Sugu alipongeza sana tena kuanzishwa kwa redio hiyo itakayopatikana Jijini Dar kupitia masafa ya 93.7 Fm na kudai sasa muda wa mageuzi umefika hivyo ni dhahiri wanamuziki wamepata mkombozi hivyo ni nafasi kwao kuanza kujipanga kwani wengi wao walikuwa wamekata tamaa ya kufanya muziki kutokana na ufisadi unaoendelea sasa kwa vituo maarufu vya radio za burudani.
Mh Komba ambae nae ni mwanamuziki ameonesha kufurahiswa kwa kufungulia radio hiyo na kusema itasaidia kuwapa vijana ajira kwani kwa sasa nchi yetu vijana wengi wana vipaji lakini tatizo linakuja namna ya kuviendeleza hivyo radio hiyo ije kwa kusaidia wanyone.

No comments:

Post a Comment