STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
“Asante Saidi kwa sababu ulionyesha kuwa una malengo makubwa na mimi mpaka sasa ningekuwa naitwa Mrs, upendo wako kwangu bado upo sanaa ila hilo ulilolianzisha kwenye kidole changu japo ndoto haikukamilika kupitia wewe litatendeka, asanteni wote mlioshiriki siku ya hili tukio akiwemo Nina na Dotnata,” aliandika Mainda.
"MJI WA DAR LEO KUZIZIMA KWA SHOO MOJA TU YA XTREME DEEJZY NDANI YA CLUB MAISHA DAR"
No comments:
Post a Comment