MAJONZI, huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia
mtoto wao mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi
mkono wa kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi
lilifuatilia.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu
usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa
marehemu huyo.
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu
Singida (DSA), alikuwa akitoka Kariakoo kununua vifaa vya kwenda navyo
chuo siku mbili mbele lakini kifo kilimkuta akiwa anakaribia kufika
nyumbani.
Kama ilivyo ada, baada ya kujulishwa tukio hilo la kikatili,
waandishi wa Uwazi walifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na baba
wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye baada ya baba mzazi
kutengana na mama yake.
Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alikuwa na haya ya kusema:
“Ilikuwa Jumamosi, Machi Mosi, mwaka huu, saa tatu usiku nikiwa karibu
na kwangu, mke wangu (mama wa marehemu) alinipigia simu akaniambia kuna
risasi zimepigwa karibu na nyumba yetu, nikamwambia haraka sana wafunge
milango na mtu asitoke nje hadi itakapojulikana kuwa risasi hizo
zilikuwa za nini.
“Muda mfupi baada ya kuongea na mke wangu, dada wa Dorryce alinipigia
simu akiniambia nirudi nyumbani haraka kwani Dorryce amepigwa risasi na
amefariki dunia.
“Nina gari, niliingia ndani yake haraka tayari kwa safari ya kurejea
nyumbani. Nikiwa nakaribia nyumbani niliona kundi la watu, nilisogelea
eneo hilo na kukuta mwili wa Dorryce umelala katika dimbwi la damu.
“Nilikuta familia yangu, akiwemo mama wa marehemu wakilia kwa uchungu.
Iinibidi nikatoe taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kitunda, nao
walinishauri niende Kituo cha Polisi Stakishari.
"IJUMAA YA KIHISTORIA NDANI YA CLUB MAISHA DAR USINGOJE KUSIMULIWA FIKA ONE BALAA LA ZUNGU MNYAMA, DVJ MAJEY NA HYPRHK"
No comments:
Post a Comment