TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, January 13, 2014

MH. KOMBA AHOFIA MAPINDUZI YA WASANII WANAOJIUNGA KWENYE SIASA!



Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh Kapteni John Komba ameonesha wasi wasi juu ya mapinduzi makubwa wanayoweza kuyafanya wasanii wanaiingia kwenye Siasa kwa sasa kwa ajili ya kugombea Ubunge.

Akiongea na Maskani Bongo Mh huyo alisema kuwa wasanii wana nguvu kubwa sana ya ushawishi ndani ya jamii hivyo kuingia kwao kwenye Siasa kutaleta mabadiliko makubwa kwenye majimbo watakayogombea.

Komba ambae kwa sasa yuko Jimboni kwake aliendelea kusema kuwa kazi ya siasa ni ya kila mmoja hivyo sula la wasanii kujiingiza ni jambo jema na kiukweli kuna baadhi ya wasanii wana nguvu kubwa sana ya ushawishi kwenye jamii hivyo mimi binafsi naamini wanaweza kufanya makubwa kwenye majimbo watakayogombea. 

Aidha Mh Komba aliendelea kueleza " Tanzania imejaliwa kuwa na wasanii wengi tu wenye nguvu za ushawishi tena mkubwa sana  bila kuwataja majina yao na kama wataamua kujiingiza kwenye siasa kwa usiliazi mkubwa basi wanaweza kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye ulingo huo wa Siasa" Alisema Komba.

Hata hivyo katika hali nyingine imeelezwa kuwa mmoja wa wasanii wanaotajwa kama watathubutu kutangaza nia ya kugombea Ubunge Wema Sepetu anaweza kushinda ushindi wa kishindo na inadaiwa msanii huyo amekuwa akifatwa sana na baadhi ya viongozi wakubwa wa Siasa majina yanahifadhiwa wakimtaka kugombea kwenye moja ya Jimbo moja Jijini Dar.
 Gazeti la Maskani Bongo lilifanya juhudi za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi ili kuzungumzia uvumi huo na kwa bahati nzuri simu yake  ilipokelewa na Meneja wake Maltin Kadinda na baada ya mwandishi wetu kutaka kufahamu juu ya ukweli wa taarifa hizo meneja huyo alijibu " Ni kweli Wema amekuwa akisumbuliwa sana na baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa wakimtaka kuchukua kadi ya unachama ili baadae aweze kugombea Ubunge" Alisema Meneja huyo 
Lakini hata hivyo meneja aliongeza kusema" Wema ni mtu ambae hapendi Siasa na wala hana mpango wa kuchukua kadi ya chama chochote ataendelea kufanya sanaa na biashara tu hadi mwisho siasa ni kazi kubwa sana" Kadinda alisem'GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI JUMATANO HII DAKA KOPI YAKO MAPEMA KUPATA HABARI ZA KINA"

No comments:

Post a Comment