Mkenye huyo asema alinusa harufu ya kifo, amfagilia Miyeyusho.
Bondia Francis Miyeyusho usiku wa mkesha wa mwaka mpya alijidhihilkisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hana mpinzani baada ya kumchakaza vibayaa bondia raia wa Kenya aliyefamika kwa jina la Joshua Amakulu.
Pambano hilo lililokuwa la kukata na shoka lilishuhudiwa na maelefu mashabiki wakiwemo waandishi wa habari ambapo kabla ya mpambano huo bondia huyo aliomba kulikuwa na tambo nyingi kwa mkenye huyo ambae rekodi yake alikuwa hajawahi kupiga hata pambano moja na siku hiyo ilikuwa mara ya kwanza kudundwa na Miyeyusho.
Maskani Bongo ambalo lilikuwepo ukumbini humo kushuhudia mtanange huo na buti ya Miyeyusho na Mkenya huyo ilianza saa 12:05: 2014 ambapo ilianza kupigwa wimbo ya taifa la Tanzania na kuatia na wimbo wa taifa la Kenya kisha mabondia hao walianza kuzipiga na kwenye raundi ya kwanza ilionesha mkenya huyo asingeweza kumaliza.
Hata hivyo usugu wa bondio huyo ulimsaidia na alifanikiwa kumaliza dakika tano zote za raundi ya kwanza, kisha iliingia raundi ya pili ambayo Miyeyusho alicharuka na kumsukumia makondo ya nguvu na yenye akili Mkenya ambae alipepesuka mara kadhaa huku akijitahidi kumkumbatia Miyeyusho ili asidondoke chini.
Zikiwa zimebaki dakika mbele tu kabla ya raundi ya kwanza kumalizika Miyeyushoi alimshindilia ngumi moja ya chembe mkenya huyo iliyompaisha juu kisha alidondoka chini na kugaragara na baada ya kuhesabiwa hadi kumi alijitahidi kunyanyuka lakini alishindwa hadi mwamuzi alipomaliza pambano hilo na kumtangaza Miyeyusho mshinda wa TKO.
Akiongea na mwandishi wetu baada ya pambano hiyo Mkenya huyo alisema " Kwa kweli nimekiona kifo any way hata hivyo sikuwa nimejiandaa nimekurupushwa tu kuja kucheza sikujua kama Miyeyusho sio saizi yangu kwa maana ya kiwango chake kiko juu na mimi bado bondi chipukizi" Alisema Joshua
Kwa upande wa Miyeyusho alisema kuwa kama kawaida yake alistahili kushinda mchezo huo kutokana na maandalizi makubwa aliyoyafanya kabla ya mechi.
No comments:
Post a Comment