Wafanyakazi wa kampuni ya Entertainment Masters Ltd ya Jijini Dar mwanzoni mwa wiki hii walionesha jeuri ya pesa baada ya kufanya party ya ina yake ambayo haijawahi kutokea nchini.
Mwandishi wetu ambae alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo alishuhudia bata za za kufa mtu ambapo kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi hao alisema kuwa chakula hicho hakikupikwa nchini bali kiliagiziwa nchini Nairobi kwa gharama kubwa.
Party hiyo iliyofanyika tarehe 3 Jumanne wiki hii ilihudhuliwa na mamia ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayomiliki Club Maisha Dar, Mbeya, Dodoma, Morogoro na Ntwara na na ilidaiwa mamilioni ya shilingi yalitumika kwa ajili ya kuwafuirahisha wafanyakazi hao waadilifu.
Hadi mwandishi wetu anaondoka ndani ya Club hiyo aliacha wafanyakazi hao wakiogelea gambe huku kukiwa na kreti kama 80 zilikuwa stoo pamoja nyingine zikiwa kwenye mafriji zikisubiri kunywewa hadi ziishe, huku mbuzi zaidi ya sita walichinjwa.
"KWA HABARI ZAIDI ZITAPATIKANA KWENYE GAZETI LAKO PENDWA LA MASKANI BONGO JUMATANO IJANYO USIKOSE"
m
No comments:
Post a Comment