Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imempiga stop Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa timu .
Akizungumza
kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph
Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi
yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha
vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya
simba.
Kingine
alichosema Itangare ni kuwa mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa
kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji..
"Kwa sasa lazima twende kikatiba, Mwenyekiti kama hayupo ngazi
inayofatia inapanda juu na tunachagua Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye
nafasi iliyobakia, kwa muda huu wa matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi
nitakaimu kama Mwenyekiti wa Simba na Swed atakaimu kama makamu
Mwenyekiti..."Alisema Itangare na kuongeza kuwa:
"Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December.
"Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December.
"Kutokana
na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi
tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor
Mahia ZDRAVOK
LOGARUSIC"
Hata hivyo taarifa hizo zimepokelea kwa shangwe kwa mashabiki wa msimbazi ambapo wameonesha kuunga mkono kamati hiyo ya kumsimamisha mwenyekiti huyo kwa madai ya kutoona mchango wake kwenye club hiyo zaidi ya maneno tu ya kuzungumzia goli tano za Yanga walizofungwa na Simba mwaka juzi.
SIKU ZINAHESABIKA ZA GAZETI PENDWA LA MASKANI BONGO KUTUA MTAANI...KAZI KWAKO MTANZANI..!!!
No comments:
Post a Comment