HII NDIO IDADI YA WAHESHIMIWA WABUNGE WATAKAOKUWEPO LEO NDANI YA CLUB MAISHA DODOMA KWENYE SHOW YA XTREME LIVE DJ DRUMMER
Kamanda wa Polisi Kanda ya DODOMA David Misime ambae ametoa baraka zote kufanyika kwa onesho hili la aina yake!
Na Livingstone Mkoi aliyeko DODOMA:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Bwana DAVID MISIME ametoa baraka zote kwa waheshimiwa wabunge kuhudhuria show iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wakazi wa Mkoa huu wa Dodoma ya XTREME LIVE DJ DRUMMER itakayofanyika leo baadae kwenye CLUB MAISHA DODOMA.
Akiongea na mwandishi wa Xdeejayz kwa njia ya simu toka nchini Uingereza ambako yuko nchini huko kikazi alisema kuwa Jeshi la polisi kanda yake limejipanga vya kutosha kusimamia usalama wa mkoa mzima na hata show hii ya leo wana taarifa hivyo waheshimiwa hao wasiwe na shaka kuhusu usalama wafike tu kwenye onesho hilo hali ya usalama imeimarishwa kwa nguvu zote.
Aidha kamanda huyo alimaiza kusema licha ya kwamba yuko mbali kikazi lakini kaimu wake pamoja na vijana wake wote watashiriki vyema kwenye onesho hilo kwa ajili ya usalama wa waheshimiwa hao ambao leo wameamua kufanya mapunziko yao kwenda kushuhudia onesho hilo ndani ya Club Maisha DODOMA. Alimaliza kusema anawatakia onesho njema waheshimiwa hao.
SUGU KUONGOZA WAHESHIMIWA:
Uongozi wa CLUB MAISHA kupitia meneja wake burudani Dizo amesema kuwa wamemteua Mheshimwa Joseph Mbilinyi kuwaongoza waheshimwa hao kwenye kuja kushuhudia mapinduzi hayo ta burudani " Tumetoa mualiko kwa waheshimiwa wote wabunge, mawaziri pamoja na makatibu wake waje kushuhudia onesho hili la kihistoria linalotarajia kufanyika leo baadae" Alisema Dizo na kuongeza kusema kuwa zaidi ya waheshimwa mia 400 wamealikwa.
DVJ MAJEY, ZUNGU MNYAMA NA HYPERMAN WATUA DODOMA ASUBUHI YA LEO KWA KAZI MOJA TU YA KUTOA BURUDANI ILIYOJE KWA MASHABIKI!
No comments:
Post a Comment