TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, September 12, 2013

WATANZANIA,KENYA WAMLILIA MH: SUGU WASIKITISHWA NA UDHALILISHAJI ALIOFANYIWA NA WALINZI WA BUNGE, POLISI NAO WASHINDWA KUMFISHA MAHAKAMANI, MBEYA WAOMBA UCHAGUZI MKUU UFIKE HARAKA WATOE MAAMUZI YAO!

 

 

JESHI la Polisi mkoani Dodoma limeshindwa kumpandisha kizimbani Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kwa madai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ alifunguliwa jalada na jeshi hilo Ijumaa iliyopita, akidaiwa kumjeruhi jichoni askari wa Bunge, Koplo Nikwisa Nkisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Wakili wake, Tundu Lissu, alisema kuwa hawakufikishwa mahakamani kama walivyotegemea kutokana na kuelezwa kuwa upelelzi haujakamilika.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa baada ya mteja wake kuripoti kituoni aliambiwa kwamba upelelezi huo ukikamilika wataitwa ili kupewa maelezo ya hatua gani inafuata.

Alisema kitendo hicho cha polisi kuwaita bila kukamilisha upelelezi wao ni kuwapotezea muda.

“Nashangaa ni kwanini tunaitwa, tuliambiwa tufike hapa, lakini tulipokuja hapa hakuna jambo lolote la maana tuliloambiwa, badala yake wanasema tuendelee na shughuli zetu upelelezi haujakamilika na baada ya wiki mbili watatuambia kinachoendelea.

“Yaani, haya mambo yanayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Naibu wa Spika, Job Ndugai, ni ya ajabu sana. Tumeitwa kutoka mbali kote kwa ajili ya kuja hapa kuambiwa kuwa upelelzi haujakamilika,” alisema.

Aliongeza kuwa Sugu alitoka Mbeya huku naye akitoka huko alikokuwa kwa ajili ya kuja Dodoma lakini hakuna jambo lolote limefanyika, na kuhoji ni kwanini wasingearifiwa hata kwa simu.

Lissu alisema kuwa atashanga kama jeshi hilo litapeleka kesi hiyo mahakamani kwani kosa lenyewe lilifanyikia bungeni.
“Nitashangaa kama jambo hili litapelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa kanuni, mbunge hatashitakiwa kwa jambo ambalo alilitenda akiwa katika maeneo ya Bunge.

“Mambo haya yalitokea tukiwa bungeni na huko kuna kinga ya mbunge. Mbunge akikosa anahukumiwa kwa mujibu wa kanuni, lakini kwa fikra na mashikinizo ya viongozi wa CCM wanataka kuvuruga na kufanya mambo kwa masilahi ya chama chao,” alisema.

Naye Sugu alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Ndugai ni cha kihuni na wala hakikuwa na misingi yoyote hadi kulazimisha askari wa Bunge kumpiga


Aidha katika hatua nyingine mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Kenya imeonesha kusikitishwa na udhalilishaji aliofanyiwa Mh; Sugu. 

Wananchi Mkoani Mbeya na mikoa mingine wamesema wanatamani uchaguzi mkuu ufike haraka ili watoe hukumu kali kwa Chama Tawala kwani wanashauhudia kila kinachofanyika mjengoni huko na wanaamini vyombo hivyo vya dola vinatumiwa kisiasa kwa manufaa ya mabosi zao waliowapa ajira.

No comments:

Post a Comment