Anti ASU (AMOS) Akiwa ndani ya kumbi za Starehe enzi zake. |
Mtaalamu huyu wa kuwabandika kope akina dada
ameuambia mtandao wa taarabuzetu kwamba ameacha kazi ya ushoga na kwa sasa
ameokoka na amesha badili jina anaitwa "AMOS".
Anti Asu
ambaye pia ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga,
inaelezwa kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumzalia watoto na
ambaye atampa mapenzi ya dhati.
Imedaiwa
kwamba, hivi karibuni Othuman alijisalimisha katika kanisa la Tanzania
Assemblies of God (TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako
alitubu dhambi zake.
Mwandishi waetu aliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo alifanikiwa kumnasa
Othuman akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo Magomeni Mapipa
jijini anakofanya kazi.
Alipoulizwa
kuhusiana na taarifa za kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli
ameacha tabia hizo na kwa sasa ameokoka baada ya kubadili dini kutoka kwenye Uislamu na kwenda kwenye Ukristo akiitwa Amos.
Anti Asu (AMOS) akicheza kwa Stail ya Pinda Mgongo. |
``Nimeokoka
kiukweli kabisa. Sitaki tena kuusikia ushoga. Nimemkaribisha Yesu awe mwokozi wa
maisha yangu. Najutia dhambi zangu na namuomba yeye (Mungu) anisimamie na
kunilinda ili nisiweze kuanguka tena,’’ alisema Anti Asu ambaye anaonekana ni
mwanaume halisi. Amesema kwamba, ameamua kuanza maisha mapya na kwamba anaishi
katika kanisa la TAG Magomeni ambako amekuwa akikesha kwa maombi.
``Mimi
nilikua shoga namba moja Tanzania baada ya marehemu Anti Kessy. Hakuna
alieyekua ananifikia. Nimevunja ndoa zaidi ya 30 na nimetembea na wanaume hata
zaidi ya 200. Nimeishi kinyumba na wanaume zaidi ya 10.
Nimebakwa
na kufanya kila aina ya ufilauni. Nani ambaye alikua ananifikia mimi?
Shoga gani ajitokeze hapa. Lakini sasa nimeachana na yote haya baada ya
kubaini nilikua naitwa na Mungu. Nimeludi kwake na ninahisi amani moyoni
mwangu,’’ amesema.
Ameongeza
kwamba kwa sasa anajiandaa kuoa kwani alipima kama ana maambukizi ya maradhi ya
Ukimwi na majibu yameonyesha kwamba yupo salama.`` Nashukuru kwamba hata jogoo
anawika.’’
Aliongeza
kwamba sababu nyingine iliyosababisha aokoke ni kutokana
na kuugua sana tangu alipokumbwa na tukio la kubakwa na wanaume zaidi ya
10.
Mchungaji
Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Dunstan kanemba amethibitisha kuokoka
kwa Anti Asu na kusema kwamba yeye ndiye aliyemuombea na kumkaribisha rasmi
kanisani hapo.
``NI
kweli Amosi (Anti Asu) tunaye hapa. Ibada ya Jumapili iliyopita tulimuombea hadharani
na alidondoka chini. Hii ni ishara kwamba alikua na mapepo yanayomsumbua.
Kanisa limempa hifadhi ya kuishi hapawakati tunamjenga kiroho.
Pia
tunamhudumia kwa mavazi na mahitaji mengine,’’ alisema Kanemba. Aliongeza
kwamba uamuzi aliofanya kijana huyo ni wa msingi na kuwataka watu wengine ndani
ya jamii wenye matatizo kama hayo kufika kanisani hapo kupata msaada wa
maombi.
``kwa
yoyote anayehitaji kumsaidia zaidi kimwili basi asisite kufika hapa kanisani.
Tunaamini kuwa kuokoka kwake kutasaidia sana kuwafanya vijana wengine wenye
tabia hiyo kuokoka pia au kuacha’’ alisema Kanemba.
Amewaasa wale mabwana zake wa zamani ambao
wamekuwa wakiendelea kumsumbua kwa kumpigia simu kwamba waache mara moja kwani
kwa sasa ameshaachana na shughuli ile.
Mtandao
wa taarabuzetu unampongeza Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni
kwa kuokoa maisha na kuamua kumjenga Kiroho Amos (Anti Asu), pia
tunampongeza Anti ASU kwa
kuokoka
No comments:
Post a Comment