Maelfu wakazi wa jiji la Dar es salaam wengi wao wakiwa ni wafuasi wa vyama vya Chadema ,Cuf na NCCR Mageuzi wemefurika katika viwanja vya jangwani kuwasilikza viongozi wakuu wa vyama hivyo ambapo kwa pamoja viongozi hao wanapinga hatua ya serikali kuingiza baadhi ya vipengele katika mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba .
Viongozi hao wanadai kuwa vipengele hivyo vitapelekea kupatikana kwa katiba ya upande mmoja na kuongeza kuwa kama mswada huo hautafanyiwa marekebisho, basi wao hawatashiriki katika bunge la katiba.
Katika viwanja hivyo ulinzi uliimarishwa kutoka katika vikundi mbalimbali vinavyomilikiwa na vyama hivyo huku shamra shamra za huko na kule zikiwa hazikosekani ili mradi kunogesha mkutano.
Mwenyekiti
wa taifa wa Chadema na ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani
bungeni Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuacha uoga na wasimame
imara kudai katiba bora.
Naye
mwenyekiti wa Cuf Mh Profesa Ibrahim Lipumba amesema Tanzani inahitaji
katiba ambayo italinda na kusimamia rasilimali za taifa kuweza kutimia
kwa usawa na kuzingatia mahitaji ya watanzania wenyewe.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbuge wa kuteuliwa amesema
hakuna haja ya kutumia mabavu na badala yake ameitaka serikali itumie
busara zaidi ili kuweza kufikia mwafaka wa jambo hili
No comments:
Post a Comment