TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, September 17, 2013

H BABA HAJIELEWI, KITENDO CHA KUVUJISHA PICHA ZA MTOTO WAO MCHANGA CHAWAKERA WATU AMBIWA AACHE USHAMBA!




 Flora Mvungi (Hadija) akijifungua.
Kutoka kwa vyanzo vyake, mbali na picha za mtoto, Mwandishi wetu alilibamba tukio la Flora akijifungua Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes iliyopo Sinza, Dar.



Flora akiwa hospitali na mumewe H. Baba.
Kwa mujibu wa H. Baba, alifurahishwa kuitwa baba kwani ni kitu ambacho alikuwa anatamani kwa muda mrefu na Mungu amemtimizia hivyo anamshukuru kwani ni zawadi kubwa katika maisha yake.

Mtoto wa Flora Mvungi.
Kwa upande wa Flora alikuwa na haya ya kusema: “Namshukuru sana Mungu kwa sababu niko salama na mwanangu, ukweli mwacheni mama aitwe mama kwani kuzaa siyo kazi rahisi”.
 
H. Baba alimalizia kwa kusema kuwa kama walivyosema awali kabla mtoto huyo hajazaliwa kuwa jina lake ataitwa Tanzanite, ndiyo hivyo itakavyokuwa jina hilo ndilo litakalotumika.

Lakini katika hali nyingine watu mbalimbali wamemponda H Baba kwa kuzivujisha makusudi picha za kitoto hicho kichanga" Huyu H Baba hajielewi kabisa kwa nini anamdhalilisha mwanae hata siku 2 hajamaliza kesha aanza kumning'iniza kwenye vyombo vya habari huu ni ushamba na upuuzi" Alisema Mama Hemed wa Kinondoni Stereo

No comments:

Post a Comment