Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema jana kuwa wameanza kufuatilia kwa undani taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la Al-Shabaab linajipanga kuishambulia Tanzania na Uganda.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),
Meja Eric Komba alisema kuwa kuna uwezekano taarifa hizo zikapikwa na
wajanja wachache kwa ajili ya kuwajengea hofu wananchi.
“Taarifa za kwenye mitandao wakati mwingine ni
uzushi mtupu… kuna kipindi ziliwekwa taarifa za uongo zinazohusu jeshi
hili,” alisema.
Alipotakiwa kutoa msimamo wa jeshi hilo iwapo taarifa hizo zitakuwa na ukweli alisema, “Jeshi tuko tayari kwa jambo lolote.”
Mtanzania ajeruhiwa
Nsanzugwako ambaye ni Meneja wa Kitengo cha
Kulinda Watoto kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Watoto
(Unicef), Kenya alisema kwamba akiwa katika Hospitali ya Aga Khan,
Nairobi alipigwa risasi miguu yote miwili.
Alisema alifikwa na mkasa huo baada ya kupitia
katika maduka hayo akitokea kazini ili kupata kahawa... “Nilipofika
baada ya nusu saa nilisikia milio ya risasi ndipo nikaona purukushani
zimeanza.”
Nsanzugwako alisema alianza kukimbia na wenzake
huku wakijaribu kuokoa watoto waliokuwepo katika eneo hilo ambao
walikuwa katika shindano la mapishi lililoandaliwa na Radio Africa
Group.
“Watoto walianza kukimbilia ghorofa za juu zaidi na magaidi walianza kuwafuata.
“Baada ya hapo, waliendelea kutukimbiza na
nilikutana nao ana kwa ana na mmoja wa magaidi hao ambaye alinifyatulia
risasi na kunipiga miguu yote miwili,” alisema.
Alieleza kwamba alijikongoja hadi alipofanikiwa kutoka nje kwa kupitia mlango uliokuwa mbele yake na kupokewa na polisi na kisha kuchukuliwa na Msalaba Mwekundu kwa ajili ya huduma ya kwanza na kisha kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
Alieleza kwamba alijikongoja hadi alipofanikiwa kutoka nje kwa kupitia mlango uliokuwa mbele yake na kupokewa na polisi na kisha kuchukuliwa na Msalaba Mwekundu kwa ajili ya huduma ya kwanza na kisha kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
“Jioni yake nilitakiwa kusafiri kwenda Geneva, Uswisi kikazi lakini kutokana na tukio hilo nilishindwa kufanya hivyo,” alisema.
Alisema amekuwa jijini Nairobi kwa miezi saba akiwa anafanya kazi Unicef.
Kaka wa majeruhi huyo, Mbunge wa zamani Kasulu
Mashariki, Daniel Nsanzugwako, alisema amekuwa akiwasiliana na mdogo
wake huyo na kwamba anaendelea vyema.
Nsanzugwako, ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni na Michezo alisema mdogo wake alimweleza kuwa tayari
ameshafanyiwa upasuaji lakini bado hajaweza kutembea.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Kenya, Shiyo Innocent ilithibitisha kuwapo kwa Mtanzania
mmoja ambaye amejeruhiwa kwa risasi katika miguu yake yote... “Ubalozi
unaendelea kufuatilia kama kuna Watanzania wengine waliokuwepo kwenye
tukio hilo.”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule alisema Serikali inaendelea
kufuatilia afya ya Mtanzania huyo.
“Ofisi yetu ya ubalozi iko karibu na inafuatilia
kila kinachoendelea. Kwa sasa nimeambiwa kuwa majeruhi anaendelea vizuri
na tuna matumaini atapata ahueni,” alisema.
No comments:
Post a Comment