JANUARY MAKAMBA ATANGAZA KUJITOA WHATSAPP
Saturday, August 24, 2013 | 2:21 PM
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
aliweka bayana kuwa ameamua kujitoa katika mtandao wa WhatsApp baada ya
kugundua haumfai.
Makamba alitoa kauli hiyo juzi, Alhamisi alipotembelea Ofisi za Global Publishers Ltd, Bamaga-Mwenge, jijini Dar kuzungumza na waandishi wa habari kupitia program mpya ya gazeti la Uwazi itakayokuwa ikiwakutanisha viongozi mbalimbali wa nchi na kufanya nao mahojiano.
Baada ya kujibu maswali mengi yaliyoelekezwa kuhusiana na wizara yake, lilifika swala la uhuru wa mitandao ya kwenye simu ndipo aliposema kuwa yeye aliamua kujitoa rasmi katika mtandao wa WhatsApp kwani hauna faida kwake.
“Nilijitoa kwa sababu niliona watu wanautumia vibaya. Utakuta hata mtu upo katika mkutano wa viongozi, ghafla unashangaa picha ya ajabu imetumwa tena kutoka kwa mtu ambaye hata haumfahamu,” alisema.
Katika mahojiano hayo, Makamba alizungumza mambo mengi yahusuyo changamoto zilizopo katika wizara anayoisimamia ambazo zitachapishwa kwa kirefu katika gazeti la Uwazi siku zijazo

No comments:
Post a Comment