MSANII wa filamu za
Kibongo, Wastara Juma hivi karibuni alikataa kuolewa na kuwa mke wa pili baada
ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja jijini Dar akimtaka awe mke
mwenzake. Wastara ambaye hivi sasa yuko Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada
ya kufiwa na mumewe, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Januari mwaka huu, alikataa
ofa hiyo na kusema kwamba kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa. Kwa mujibu wa
chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kushauriana na
mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia yao. “Mwenyewe alisema
alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara kuwa mke mwenzake kwa sababu
imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza chanzo hicho.
UTHIBITISHO NI
HUU Baada ya kuzinyaka habari hizo, kama kawaida yate lilimnyanyulia mkonga
mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, akathibitisha kumpigia
Wastara. “Lengo langu lilikuwa zuri tu, unajua dini yetu ya Kiislamu
inaturuhusu kuolewa wanawake mpaka wanne hivyo niliona ni heri nikae na
mwenzangu. “Halikuwa suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na
tulishajipanga kwenda kutoa mahari kwao. Nimesikitika sana alivyokataa ila
namtakia kila la heri katika maisha yake,” alisema.
WASTARA SASA “Ni
kweli nilipigiwa simu na mwanamke wa huko nyumbani (Tanzania), nilimjibu kama
ninavyokuambia wewe sasa hivi, kwamba sifikirii kuolewa kwa sasa,” alisema
Wastara kwa njia simu alipopigiwa na mwandishi wetu.
No comments:
Post a Comment