Umati mkubwa wa mashabiki ulihudhuriwa na maelfu ya watu kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jumapili iliyopita.
Mwanamuziki Madee akifurahia shoo hiyo muda mfupi kabla ya kwenda kuwarusha mashabiki wake waliokuwa wamemwagia pombe yake.
Mtangazaji wa Redio Times Edson Mkisi akimuhoji mmoja wa wanamuziki uwanjani hapo.
Natasha & Monalisa wakiingia kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kushuhudia tukio la kihistoria la moja ya shoo zilizoandaliwa na kituo hicho namba moja.
Mwanamuziki Juta B anaetamba na wimbo wa "Bint Mtwara" ambae pia ni mfanyabishara wa matunda kwenye soko la Tandika akiwa ndani ya viwanja hivyo kushuhudia shoo hiyo iliyofana.
Juta akiwa na shabiki wake kwenye viwanja hivyo.
Na Livingstone Mkoi
Kituo namba moja kwa sasa cha burudani na habari Radio Times mwishoni mwa wiki iliyopita ilifanya tukio la kihistoria ambalo ni dhahili kuwa sasa kituo hicho kitafuka kila idara siku za usoni kwa kufanikisha kuandaa tamasha kubwa la wazi huku watu zaidi ya elfu therathini wakihudhuria.
Mapapalazi wa Xdeejayz waliokuwepo uwanjani humo walishuhuduia msitu wa watu waliokuwa wamefurika uwanjani humo huku idara ya usalama na ikiimarishwa kila kona kuhakikisha hakuna mwananchi anaeporwa na hakika waliweza kuthibiti hilo.
Shoo hiyo iliyokuwa na wasanii kibao wakiwemo Ney wa Mitego,Diamond, Mad na wengineo na wasanii wote hao walitoa burudani ya aina yake ambayo ilikidhi haja ya mashabiki.
No comments:
Post a Comment