TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, January 8, 2013

MZEE MAJUTO ATOA SABABU ZA KUTOHUDHURIA AROBAINI YA SHAROMILIONEA!

 KING MAJUTO & SHARO MILIONEA.
MZEE MAJUTO AKIWA PEMBENI MWAA GARI YAKE.

Na Livingstone Mkoi
Mfalme wa kuchekesha nchini Othuman Majuto "King Majuto" ametoa sababu za msingi ambazo zilikuwa juu ya uwezo wake za kushindwa kwenda kushiriki kwenye arobaini ya Sharo Milionea iliyofanyika mwishoni tarehe tano mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akiongea kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi King Majuto alisema kuwa"Kweli nilijisikia vibaya kwa kutofika kwenye arobaini ya mwanangu Sharo kutokana na kusumbuliwa na malaria ya kali" Alisema Mzee Majuto
Aidha Mzee Majuto aliongeza kusema pengo la Sharo kwake haitokuwa rahisi kufutika katika maisha yake kwa vile aliishi na Sharo kama mwanae kwa miaka mingi huku akimuheshimu kama babaake mzazi.
Hata hivyo Majuto alimaliza kusema kuwa kwa sasa afya yake inaendela vyema hivyo mashabiki wasiwe na shaka kuhusu afya yake kwani yuko anaendelea vyema na hivi karibuni atarejea kwenye shughuri zake za sanaa,ambapo 2013 amewaandalia mambo mazuri watanzania wao wakae mkao wa kula tu.

No comments:

Post a Comment