TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 23, 2012

WEMA SEPETU ADAIWA KUITELEKEZA FILAMU YAKE STUDIO !

Ni ile aliyoizindua kwa mbwembwe mwezi wa sita mwaka huu.

 

Filamu ya aliyekuwa Miss Tanzania 2006/7 Wema Sepetu iitwayo" Super Star"ambayo mwezi Juni mwaka huu aliifanyia uzinduzi wa kufa mtu imedaiwa kutelekezwa studio huku ikiwa bado haifaisha baadhi ya vipande.

Habari za uhakika ambazo hazina chembe ya uongo zilisema kuwa filamu hiyo inayotengenezwa na Prodyuza aliyefahamika kwa jina la Chid iko studio tu kama haina mwenyewe" Ni kweli jamani hiyo filamu ni kama imetelekezwa flani kwani mtu mwenyewe Wema hana mpango wowote nayo muda unazidi kwenda wala haihangaikii kumalizia vipande vilivyobaki" Alisema mmoja wa rafiki wa karibu na Wema

Hata hivyo kona hii ilimtafuta mtengeneza filamu hiyo ili kuweka wazi kulikoni msanii hiyo kuiacha filamu hiyo kwa kipindi chote hicho wakati alitumia mamilioni ya pesa kuitengeneza, Ambapo Chid alifunguka namna hii" Kaka ni kweli hii filamu bado ipo mikononi mwangu kwanza kuna utofauti kidogo mimi na Wema hivyo tunahitaji kumalizana mambo flani ndipo niimalizie filamu yake vinginevyo itaoozea hapa" Alisema Prodyuza huyo bila kufafanua ni mambo gani ya kumalizana na Wema

No comments:

Post a Comment