Vurugu zilizofuatia mtoto aitwae Emmanuel Josephat (14), Kukuojolea msahafu (Quran) zimechukua sura mpya baada ya baadhia ya waumini wa dini ya kiislam kukusanyika na kushinikiza mtoto huyo aachiwe na polisi ili wamuue.
Waumini hao wanaokadiriwa kifikia idadi ya watu 3000 baada ya kutawanywa na polisi waliingia mitaani na kuchoma moto kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mbagala Zakhem, wakaharibu Kanisa la Anglican, wakavunja vioo vya kanisa la wasabato, na kuchoma moto Tanzania Assembly Of God (TAG) la mbagala Mbagala kizuiani na kuchukua vifaa vya muziki vya kanisa hilo...
Awali waumini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi cha maturubai, Mbagala kizuiani wakitaka mtoto huyo ambaye alikuwa nchini ya ulizi wa polisi aachiwe, na polisi walipokataa matakwa yao ndipo vurugu hizo zilipoanza.
Chanzo cha Tukio hili ni mabishano baina ya watoto wawili, Emmanuel Josephat, na mtoto mwingine wa kiislam, kwa jina hatujalifahamu
Jeshi La FFU wakiwa wanajaribu kutuliza Fujo
Mmoja wa waandamaji akiwa amekamatwa na FFU
Hawa Ndio Baadhi ya waandamaji waliokamatwa wakiwa wanapandishwa kwenye Gari ya polisi
Baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamekamatwa na Polisi
Polisi wa Jeshi la FFU wakiwa katika harakati za kutuliza fujo za waandamanaji
Moja ya Gari la Raia lililo haribiwa
Mmoja ya kanisa yaliyo haribiwa huko mbagala
No comments:
Post a Comment