TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, October 27, 2012

SIASA - UCHAGUZI UVCCM TAIFA NA DHAMBI YA MPASUKO



SIASA:     Katika hali isiyokuwa ya kawaida Vijana wa umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuingia   katika mgogoro mkubwa na mzito miongoni  mwa vijana hao katokana na Uchaguzi  uliofanyika tarehe 24/10/2012 na matokeo kutangazwa tarehe 2510/2012. Haki haikuwa shwari kutokana na baadhi  ya wapiga kura kutokubali matokeo hayo ya viongozi  waliopigiwa kura. Miongoni mwa sababu zilizosababisha mgogoro na mpasuko mkubwea  ndani ya umoja huo imala hi pamoja na matumizi ya fedha yaliyojitokeza kwa wagombea wote. Hakuna mgombea hata mmoja ambaye amegombea nafasi hiyo ya Umwenyekiti na   umakamu Mwenyekiti ambaye hakutumia hata chapa kuhakikisha anapata fursa ya kuongeza jumuiya hiyo. Kila mgombea kutoa fedha isipokuwa wametofautiana utoaji wa fedha na mbinu za kiufundi  hali iliyopelekea walioshinda wakashinda na walioshindwa wakashindwa. Matumizi hayo ya fedha ndani ya uchaguzi wa jumuiya yasipoangaliwa kwa umakini  yatavunja jumuiya kwa kiasi kikubwa sana kauli ya Mheshimwa Rais  na Mwenyekiti wa chama juu ya kupiga vita matumizi ya fedha imepuuzwa kwa kiasi kikubwa sana.
       Suala hili litazamwe kiutendaji na watu sio kisiasa.Sababu  nyingine ni madalali wa kisiasa,kwa kiasi kikubwa madalali hawa wamekuwa tatizo kubwa sana katika chaguzi za vyama vya siasa.Watu hawa hawapigi kura  kazi  yao  ni kuwaimba na  kuwanadi wagombea. Malengo makubwa ya madalali  hawa wa saisa  ni kuwasaidia wagombea ili baadaye wapate fursa za kuteuliwa ndani ya jumuiya au chama. Hawa wamekuwa chanzo cha migogoro matusi na kuchochea vurugu na fujo kubwa ndani ya CCM . Suala hili ni chanzo kikubwa ndani ya jumuiya ya umoja wa vijana.
      Vilevile ni ukomavu mdogo wa kisiasa kwa kiasi furani vijana wa UVCCM hawajakomaa kisiasa. Ukomavu wa kijana wa CCM kideomkrasia ni lazima ukubali kushinda na ukubali kushindwa katika uchaguzi  kitendo cha mgombea kutokukubali kuwa  ameshindwa ni tatizo kubwa lililopelekea mgogoro ndani ya UVCCM  mfano ni pale Paul Makonda aliyekuwa akigombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM alipopewa fursa ya kushukuru baada ya  matokeo kutangazwa na kushindwa alisema “Ni bora kushindwa kishujaa kuliko kushinda kwa fedheha”. Hii ni kauli ya mtu ambaye bado hajakomaa kisiasa. Pia kitendo cha Paul Makonda kukataa  nafasi ya ujumbe wa baraza la Taifa UVCCM ambayo aliteuliwa na Mwenyekiti wa UVCCM  Sadifa kutoka  katika nafasi zake tatu ni ushahidi kuwa hakustahili hata kugombea fursa hiyo ya  umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa
Viongozi wa chama kuwekeza katika jumuiya mitaji yao kisiasa kwa ajili ya matumizi      
ya nyadhifa  hizo  za vijana kwa ajli kuonesha namna  gani wanakubalika katika chama na jumuiya zake.
        Pia tatizo lingine ni namna Mwenyekiti wa  UVCCM Taifa na makamu wake wanavyopatikana tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi mapema  siku za usoni litaleta tatizo kubwa sana kwa mujibu  wa kanuni za UVCCM ibara ya 95 inaeleza  kuwa kama Mwenyekiti akitoka Tanzania bara basi makamu wake atatoka Tanzania Visiwani (Zanzibar) au  kinyume chake. Hili ni tatizo kubwa    linaloonesha kuwa hakuna Utanzania katika kuunda Uongozi wa Jumuiya bali kuna Ubara na uvisiwa ambao sasa  umeleta ukunda., Maana na wao wanataka nafasi  ya  makamu au Mwenyekiti wa jumuiya atoke kanda ya ziwa na hakuna hata Mjumbe mmoja wa NEC aliyetoka kanda ya ziwa katika mikoa ya Kigoma, Mwanza, Kagera,Mara,Shinyanga,Singida,Tabora  kati ya wajumbe wote sita waliopigiwa kura.Hoja hii inapaswa itatuliwe kidiplomasia zaidi kuliko maandamano na vurugu katika jumuiya.Hali kama hii inaashiria kupasuka kwa umoja wa kitaifa na itapelekea kuibuka kwa dhana ya ubaguzi wa kijiografia . Watu wa kanda ziwa hawapaswi kulaumu kwa kukosa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au MNEC  wa jumuiya maana maltine shigera ni mtu wa kanda ya ziwa ambaye ndiye katibu mkuu wa UVCCM. Pia kauli za viongozi wastaafu wa CCM na serikali wamechangia  kwa kiasi kikubwa kuwaandaa vijana kisaikorojia kukubali kuwa wanaonewa kutokana na kauli za viongozi hao baada ya kudondoshwa katika nafasi walizogombea katika chama.

MALIKI MARUPU MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA.


No comments:

Post a Comment