TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, December 12, 2013

UWAZIRI MKUU MGUMU SANA JAMANI-MIZENGO PINDA HATA LEO HII IKITOKEA RAIS AKANIAMBAI.....!!!!




  Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita  kwamba kama ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye  atafurahi sana  kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.



" Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo.
"Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata  wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO Rais  akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi," amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.




Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia aliyetaka  kujua  msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri  kutokana na ufisadi wa kutisha  TAMISEMI.
"ZUNGU MNYAMA AWAAHIDI MAKUBWA WAKAZI WA MOROGO KWENYE UZINDUZI WA CLUB MAISHA NI TAREHE 19-20 MWEZI HUU"

No comments:

Post a Comment