TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, November 27, 2015

MASKINI YA MUNGU WEEH: MKUU WA WILAYA KINONDONI AFANYIWA UMAFIA WA KUTISHA, RAIS MAGUFULI, WAZIRI MKUU WAOMBWA KUMSAIDIA HARAKA ILI KUNUSURU UHAI WAKE. MASKANIBONGOTZ YANASA TAARIFA HII NYETI YA KUSIKITISHA!


Rais Dokta John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa ambapo viongozi hawa wakuu wameombwa na wananchi kumuongezea nguvu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda ili afikie malengo yake ya kumaliza mgogoro huo wa Ardhi kwa amani huko Kata ya Wazo kwenye vitongoji vya Nakalekwa na Nakasangwe. Kwani changamoto kubwa aliyonayo Mkuu huyo wa Wilaya inadaiwa kuwa kwenye mgogoro huo yuko Kigogo mmoja mzito mwenye mamlaka kuliko yeye aliye upande wa mafisaidi. maskanibongotz
Mlinzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akisogea karibu na mlango kwa ajiri ya kmufungulia ili aishuke kwenye viwanja vya Nakalekwa CCM siku ya jana tarehe 26.. maskanibongotz
                               
Mh Paul Makonda . maskanibongotz

Hii ndiyo shughuri aliyokutana nayo Makonda jana huko Nakalekwa  maskanibongotz



Hapa DC huyo akiwaombea msamaha kwa kuhiswa vibaya watumishi hao na kuwahisi watu wamesiwe na shakana kuhusu zoezi hilo kuwa litakwenda vizuri kwa baraka za Mungu. maskanibongotz


Na Mwandishi wa maskanibongotz
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua, Hali ya usalama ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kwa sasa huenda ikawa mashakani baada ya kujitoa muhanga kupamba na ufisadi mkubwa unaofanywa na matajiri wenyewe mgogoro wa ardhi na wananchi wanyonge kwenye Kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe na Nakalekwa, huku nyuma ya matajiri hao kuna vigogo wakubwa wa Serikali wenye nguvu kuliko yeye.
Habari za uhakika toka kwa vyanzo vyetu makini ambavyo havina hata chembe ya shaka viliuleza mtandao huu wa maskanibongotz kuwa Mkuu huyo wa Wilaya ambae amekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge hasa wanaoonewa kwenye masuala haya ya ardhi lakini mtihani mkubwa uliopo ni nguvu ya pesa kwani mafisadi wamewakamata watu wa mipango miji Manspaa ya Kinondoni, Watu wa Ardhi na hata msaidizi wa Dc huyo.
Mkuu huyo wa Wilaya wiki hii tarehe 25 mwezi huu ilikuwa anye mkutano na wakazi hao wa Nakasangwe na Nakalekwa ilikuwa kwa ajiri ya kuwaeleza wakazi hao namna alivyofanya jitihada za ziada kufanya vikao na pande zote mbili yani viongozi wa Serikali ya mtaa huo akiwa na kamati iliyokuwa imeteuliwa kwa ajiri ya kusimamia  vikao vya usuruhishi lakini pia timu ya pili ni ile ya watu wanaodai kuwa maeneo hayo wanayoishi wananchi ni yao.
Hata hivyo vikwazo vilianza kuingia baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kufika kwa muda mrefu huku akiwasubiri maafisa Ardhi ambao walidaiwa walikuwa wametokea kwenye kikao cha siri na mafisadi hao kwa lengo la kukwamisha zoei hilo lisiende sawa kama lilivyokuwa limepangwa ambapo baadae walipofika maafisa hao kumi na moja Dc huyo aliamuru kuwaweka ndani kwa uzembe walioufanya lakini si hivyo inadaiwa mkuu huyo wa Wilaya nae alikuwa amepata taarifa za wapi walipokuwa wamepitia.
Kwa siku hiyo ya tarehe 25 zoezi hilo lilikwamba ambapo Mkuu wa Wilaya alimuagiza Mwenyekiti wa Nakasangwe Peter awaombe radhi wananchi kwa niaba yake kwa tukio lililokuwa limetokea na kuahidi zoezi hilo kuendelea kesho yake ambayo ni jana tarehe 26.
Hata hivyo siku hiyo ya jana wakazi hao zaidi ya elfu 30 walikusanyika mapema sana kwa ajiri ya kumsubiri Mkuu huyo wa Wilaya ili wamsikilize ambapo mapema tu kiongozi huyo anaechukia rushwa alifika akiwa ameongozana na wale maafisa Ardhi na watu wa mpango miji, Rpc Wambura na wale watu wa upande wa pili wanaodai maeneo hayo ni yao.
Baada ya kufika  eneo la uwanja wa CCM Nakalekwa Mkuu huyowa wilaya alikutana na mabango yenye jumbe za kushtua ambapo mabango hayo yaliyokuwa yanasema kuwa wakazi hao hawana imani na watu wa mipango miji kwa vile kuna taarifa wanashirikiana na  mafisaidi, huku pia wakazi hao wakimkataa moja kwa moja DASI msaidizi wa Mkuu wa Wilaya kwa madai kuwa yumo kwenye mtandao wa  kushirikiana na mafisadi hao ili wawadhurumu wakazi hao ardhi yao.
Sehemu hiyo mabango pia ili muomba Rais Dokta John Pombe Magufuli kuwashughurikia watu wa Mipando Miji na maafisa Ardhi kwa ufisadi na mambo mengine mabango hayo kama yanvoonekana pichani, hata hivyo hali hiyo ilimshtua Mkuu huyo wa Wilaya na kuwasihi wakazi hao kuwaamini maafisa ardhi wake kwani nay eye atakuwepo kwenye zoezi kwa siku za awari jambo ambalo lilipingwa vikali na wakazi hao kwa kuonesha wasi wasi wao kuwa endapo wakiachiwa maafisa ardhi hao peke yao bila yeye Dc huenda zoezi hilo lingeleta utata na ndichp kilichotokea leo tarhe 27.
Zoezi hilo kwa jana alilienda swa kwa vile Mkuu wa Wilaya alilisimamia vizuri lakini siku ya leo tarehe 27 zoezi hilo limeshindwa kuendelea baada ya watu wanaodaiwa kuwa ndiyo wenye mashamba ambao kwa awali walikuwa hata 20 hawafiki lakini siku ya leo wameongezeka na kufika zaidi ya 60 huku wakitaka nao waorozeshwe kwenye uhakiki wa viwanja hivyo.
Hali hiyo ikatibua mambo kwani japo la wajumbe wa nyumba kumi wakiongozwa na mwenyekiti Peter waligoma matakwa ya upande huo wa pili kutaka kupachikwa watu hao ambao hwatambuliki, lakini hata hivyo katika hali ya kushangaza maafisa Ardhi hao wakiongzwa na Seif walikuwa wanalazimisha watu hao wasiofahamika wawekwe tu ili zoezi liendelee.
Msimamo mkali wa mwenyekiti wa Serikali za mtaa na kamati yake kuwakataa watu waliokuwa wamepandikizwa ndiyo umepelekea watu wa ardhi kuchukia pamoja na wale wa upande wa mafisadi kuamua kuondoka eneo la viwanja hivyo na kupelekea zoei la uhakiki kusimama kuanzia leo hadi wananchi hao watakapotangaziwa tena.
JUHUDI ZA MAKONDA ZINAVYOKWAMISHWA NA KIGOGO MWENYE NGUVU KULIKO YEYE.
Katika jitihada za mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kwa amani na isitokee tena watu wakauna kama katika eneo hilo zinadaiwa kukwamishwa na mtandao mkubwa ulimzunguka Makonda ambao ukiongozwa na Mkuu wake wa kazi mwenye nguvu kuliko yeye huku akiwapa nguvu watu wa Mipango miji, maafisa Ardhi, pamoja na msaidizi wake ambae wakazi hao wanasema hawataki kumuona kwa vile wanajua kila kinachoendelea kuhusu mgogoro huo.
Changamoto nyingine anayokutana nayo DC huyo ni kwamba mgogoro huo ameukuta unaendelea na mbaya zaidi baadhi ya watumishi wa Manisptaa wenye kitndo cha Ardh na Mipango miji wamekuwa sehemu ya mgogo huo na inadaiwa walishavuta pesa ndefu toka kwa mafisadi hao ili kuhakikisha wanapata eneo hilo kwa nguvu yoyote.
Bahari zaidi toka kwa vyanzo hivyo viliendelea kuueleza mtandao wa maskanibongotz kuwa  maafisa hao wanatajwa kwenye kashfa hiyo wametokea kumchukia DC MAKONDA kwa kitendo chake cha kuonesha kuwatetea wakazi hao  hali inayopelekea kushindwa kumpa ushirikiana na kama wanampa basi kwa shingo upande, na mbaya zaidi yupo kigogo mmoja ambae ana sauti kuliko Makonda kutokana na  kuwa karibu na mafisaidi hao wanaodaiwa kumwaga pesa kama mchanga.
Hali hiyo sasa inapelekea zoezi hilo kuwa na ugumu kutokana na maafisa mipango na Ardhi kulindwa na boss wake Makonda, hata hivyo wakazi hao wa NAKALEKWA na NAKASANGWE walionesha wasi wasi wao na hali ya usalama wa Mkuu wao wa Wilaya juu ya jambo hili kwani tayari kwa sasa Dc huyo yupo kwenye vita kubwa kupambana na boss wake, watu waliochini yake na mafisadi/
Kufuatia hali hiyo wananchi mbali wanaofatilia mgogoro huu wa kipindi kirefu wamemuomba Rais Dokta John Pombe Magufuli kumuongezea nguvu DC Makonda kwenye sula hili kwa vile hali ya usalama juu ya jambo hili kwa sasa kuwa mbaya kwani mkuu huyo anapambana hadi na bosi wake kikazi ambae anadaiwa kuwapa nguvu watu wa ardhi na mipango miji kuhakikisha wanakwambisha hili jambo.
Habari zaidi zilisema kuwa hata siku Makonda alipowaweka ndani watu hao wa Ardhi kwa amri ya kutowaachia hadi kwa amri yake dakika chache baadae ilidaiwa boss wake Makonda alipiga simu na kuamuru waachiwe haraka maafisa ardhi hao.
Kigogo huyo pia amewahi kusababisha mgogoro wa watu wa gereji pale Tegeta kwa kutaka kuwahamisha watu hao hali iliyozusha balaa kubwa kwani kigogo huyo ana rafiki yake muhindi ambae ndiye aliyekuwa anapataka pale kwa watu wa magereji si kama alivyokuwa ametangaza kuwa wamevamia eneo la hifadhi.
Mtandao huu unaungana na watanzania wapenda amani, wapenda haki kuiomba Serikali Kuu kwa maana ya Waziri Mkuu , Majaliwa Kassim Majaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Dk John Pombe Magufuli kusikia kilio cha wapiga kura wake, lakini pia kuchunguza tuhuma hizi zinazowakabiri maafisa Ardhi, Mipango Miji na msaidizi wa DC Kinondoni ili kama zina ukweli ndani yake basi wachukuliwe hatua haraka ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Mwandishi wa maskanibongotz  siku ya aleo alifika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni kwa ajiri ya kuzungumza na Mkuu huyo wa Wilaya kuhusu changamoto hizo na tuhuma zinazowakabir maafisa wake wa ardhi na mipango miji hadi wananchi kuwakataa lakini mkuu huyo hakuwepo ofisini na tulielezwa yupo nje ya ofisi kwa kwa majuku ya kiofis.
Credit:maskanibongotz

No comments:

Post a Comment