TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, August 10, 2015

MASIKINI YA MUNGU: WASANII RAY NA JB KWISHA HABARI YAO. KAZI ZAO ZASHUKA CHINI YA KIWANGA KWA 43%, KAMPUNI YA STEPS HUENDA IKASITISHA MKATABA NAO..!%



 Msanii wa tasnia ya filamu Tanzania Jakob Steven JB ambae kwa sasa imelezwa kuwa kiwango chake cha kuigiza kimeshuka sana kiasi cha kupoteza mvuto kwa mashabiki  huku kukiwa na taarifa kuwa huenda kampuni ya usambazaji filamu ya Steps ikampiga chini kwani kazi zake haziuzi kabisa huku zikiwa zimekosa ubunifu. Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema kuwa sababu ya kushuka kisanaa kwa Jb ni kutokana na kuridhika na kulewa ustaa wa kibongo bongo bila kutambua kama Watanzania wengi walimtegemea yeye baada ya kifo cha Kanumba lakini hadi sasa anazidi kurudi nyuma baada ya kupanda ili kuifikisha sanaa ya bongo kimataifa.
 Vicent Kigosi Ray ambae nae kwa sasa anapumulia mashine kutokana na kazi zake kushindwa kufikia malengo ya kimataifa na hajawahi kufanya kazi yoyote iliybamba Afrika Mashariki zaidi ya kazi alizowahi kufanya na rafiki yake Marehemu Steven Kanumba na kufanikiwa kuzikonga nyoyo za Wakongo pamoja mashabiki wa Afrika Mashariki na Kati
Sababu nyingine ambayo imemfanya Ray kushuka kwa kiwango chake kiasi cha kuzidiwa hata na msanii chipukizi Manaiki Sanga ambae hana hata miaka mitatu kwenye sanaa, ilidaiwa kulinga kwa msanii huyo na kujiona amemaliza kazi kwa kujurikana Tanzania, baadhi ya waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari waliofika kwenye uzinduzi wa Club Maisha Basement hivi karibuni walikera na tukio la msanii huyu kugoma kupigwa picha na waandishi ili hari siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajiri ya watu maarufu kwa Tanzania, huku msanii mwenzake Jb akikubari kupigwa picha.
 Filamu ya Going Bongo ya msanii Ernest Napoleon ambae ni mtanzania aishie nchini Marekani ambayo hivi karibuni ilizinduliwa Zanzibar kwenye tamasha la maonesho ya Filamu ya nchi za Majahazi ZIFF na kushinda tuzo maalum ya filamu bora Afrika Mahariki na kati. Filamu hii imeonekana kuchangia kuwamaliza Jb na Ray kwani imekuwa filamu ya kwanza kuigiza kwenye nchi za Marekani na Tanzania na kushirikisha wasanii wengi huku gharama yake usipime.
 Ernest Napoleon
 Ernest Napoleon katika tuzo huko Zanzibar
 Ernest Napoleon akiwa kwenye uzinduzi wa filamu yake nchini Marekani ambapo filamu hiyo ya Going Bongo hadi sasa imekwisha zinduliwa zaidi ya nchi 7 Duniani.

 Libert Msuya mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania ambae ni rafiki wa karibu na Ernest Napoleon ambae nae ni msanii wa Bongo Movie mwenye malengo ya kuifikisha sanaa ya Tanzania kimataifa na sio kutaka kujulikana hapa hapa nchini kama wafanyavyo mastaa wengine.
 Hii ndiyo demo ya filamu ya msanii Manaiki Sanga bofya hapa kuiona
 
Msanii Manaiki Sanga the Don ambae nae ameleta mapinduzi makubwa kwenye sanaa ya Tanzania kwa kufanya movie ya kimataifa ambayo haijawahi kufanywa na msanii yeyote tangu tasnia ya filamu ianze nchini.Manaiki ambae ndiye staa wa filamu ya Wake Up ambayo amewahenyesha wasanii mastaa zaidi ya 3o wa bongo movie huku filamu hii ikiwa ni ya pili kwake ambapo miaka 3 iliyopita alitoka na filamu ya Ngema ambayo nayo ilibadilisha soko la filamu Afrika Mashariki na kati na kuwa filamu iliyonunuliwa na watu zaidi ya laki 9 na elfu tisni. Hata hivyo kwenye hii filamu ya Wake Up ambayo inatarajia kutoka mwisho wa mwezi huu na kwa maelezo zaidi unaweza kumfollow Manaiki Sanga kwenye Instagram
Ernest Napoleon
Na Hii ni Demo ya Filamu yake ya Going Bongo ebu icheki

 

No comments:

Post a Comment