HII NDIYO FILAMU YA GOING BONGO YA MTANZANIA ANAEISHI NCHINI MAREKANI AMBAYO KWA SASA HIVI IMEKUWA GUMNZO KUTOKANA MSANII HUYO KUONESHA KIPAJI CHA HALI YA JUU KIMATAIFA
Msanii Ernest Napoleon akipokea tuzo mara baada ya filamu yake kushinda na kuwa filamu bora Afrika Mashariki na Kati.
Msanii Ernest Napoleon staa wa filamu ya Going Bongo akiwa ndani ya filamu hiyo iliyooneshwa zaidi ya nchi 7 Duniani.
Msanii Ernest Napoleon akiwa mzigoni
Na Mwandishi Wetu
Filamu ya kimataifa ya Going Bongo iliyoandaliwa kwenye nchi za Marekani na Tanzani huku msanii toka Tanzania Ernest Napoleon akionesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwachanganya mashabiki waliofurika kwenye tamasha la ZIFF kushuhudia kuiona filamu hiyo kwa mara ya kwanza.
Filamu hiyo ambayo siku ya Ijumaa wiki iliyopita ilioneshwa kwa mashabiki zaidi ya elfu mbili waliokuwepo kwenye utoaji tuzo kwa Filamu mbalimbali, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mashabiki wengi walionekana kukunwa na msanii Ernest Napoleon ambae ana kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwafanya watazamaji kushindwa kuamini alichokuwa anakifanya msanii huyo.
Katika maonesho hayo filamu hiyo ilifanikiwa kuchukua tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki na Kati huku mashabiki wengi wakitamani kupata nakala ya filamu hiyo ya kimataifa, aidha muandaaji wa filamu hiyo ambae ni Ernest Napoleon alisema kuwa filamu hiyo kwa sasa imeshaoneshwa kwenye nchi nyingi za kimataifa kama vile Uingereza, Italia, Marekani, Ujerumani, Nigeria na nchi Afrika Kusini itafatia hivi karibuni.
Filamu hivyo kwa nchi ya Marekani sehemu kuwa imeigiziwa kwenye Hospitali ya 'Beverly hills medical center' iliyopo mjini Los Angeles huku kampuni za Busy bee production na Ronald brothers production zikisimamia uchukuaji video, huku waigizaji waliotoana jasho ni ; Ernest Napoleon,Emanuel Galliusi,Ashely Olds,Nyokabi Gethaiga huku ikiongozwa na Leslie Bumgarner, Dean Ronald's, na imendaliwa na Ernest Napoleon,Nick Marwa na Dean Reynolds.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umegundua kuwa staa huyo amekuwa dili kwa watoto wazuri wa kike Jijini Dar wakiwemo mastaa wa kike ambapo amekuwa wanted kila kona hali iliyomfanya staa huyo mnyamwezi kukimbilia Zanzibar kujificha.
No comments:
Post a Comment