rais wa Ujerumani Bw. Joachim Gauck amezitaka nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha ushirikiano miongoni mwao.
Ushirikiano huo unahusisha kukabiliana na changamoto zilizopo
pamoja na kuimarisha misingi ya haki za binadamu.
Aidha, Bw. Gauck amesema hayo baada ya kuhitimisha ziara yake hapa nchini kwa kutembelea makao makuu ya mahakama ya afrika inayoshughulikia haki za binadamu na jumuiya ya Afrika Mashariki zote zilizoko jijini Arusha.
Naye Rais wa mahakama ya Afrika jaji mstaafu Agustino Ramadhani na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Richard Sezibera wamesema ziara hiyo imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano na imeongeza chachu ya maendeleo.
Kwa upande mwingine Rais huyo amemaliza ziara yake nchini Tanzania kwa kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhamasisha watalii kutoka nchini Ujerumani.

No comments:
Post a Comment