Taarifa mpya ya sasa inasema Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa katoliki nchini humo kumuita Mungu ‘Allah’ kwenye gazeti hili linaloandika habari zake kwa lugha ya Ki malay.
Walidai
kuwa Wakristo wanawakanganya Waislamu walio wengi na hilo laweza
kuhatarisha usalama wa taifa ambapo uamuzi wa Mahakama ni mojawapo
ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki
zilizochukua muda wa miaka saba na kusababisha mashambulizi katika
makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh mwaka
2010.
BBC
wanaripoti zaidi kwamba Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa
wakimwita Mungu ‘Allah’ katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda
mrefu sana.
Mahakama
nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa
katika ukristo ambapo mgongano huu kuhusu neno hilo moja umedhihirisha
jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofautitofauti lilivyogawanyika.
Wanaharakati
wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya Mahakama huku wengi
wao wakiwa wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu ‘Allah’ kama njia ya
kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo wamekana.
No comments:
Post a Comment