Mkuu wa jeshi la polisi nchinivia
Imma Matukio — Jambazi mkuu anayetuhumiwa kujihusisha na matukio ya
mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyo tokea Wilayani Tarime
kuanzia 26 hadi 28.01.2014 amekamatwa na jeshi la polisi jioni ya Tarehe
06.02.2014 mkoani Tanga.
Akisimulia
kukamatwa kwa jambazi huyo Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya
Justus Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jioni ya Tarehe
06.02.2014 majira ya saa 1.30 na katika mahojiano
ya awali ya jeshi la polisi mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na matukio
ya mauaji ya kuanzia tarehe 26 hadi 28 na unyang’anyi wa kutumia silaha
pamoja na mengine.
Kamugisha
alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw. Chaerles Range Kichune, 38 maafuru
kama Josephat Chacha ama Joseph Charles Chacha Msong’o mkazi wa
Kenyamanyori kata ya Turwa Wilayani Tarime.
Aidha
Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa alimtaja Marwa Keryoba Alex 30 – 38
mkazi wa Kijiji cha Kebeyo Sirari Wilayani kuwa wanashirikiana kufanya
ujambazi na silaha ametunzia nyumbani kwake huko Musoma.
‘“Polisi
baada ya kupata taarifa hizo walifuatilia hadi nyumbani kwa mtuhumiwa
ambapo walimkuta na alipo waona maasikari polisi alijaribu kukimbia huku
akiwa amebeba silaha aina ya (bunduki) SMG .Askari walipiga risasi
hewani wakimtaka kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kuwarushia
risasi na ndipo asikari waliendelea kurushiana risasi na hatimaye
kumpiga risasi, marehemu alifia njiani akiwa anapelekwa hospitalini kwa
matibabu,” alisema Kamugisha.
Kamugisha
ameendelea kusimulia kuwa marehemu alikutwa akiwa na Bunduki anina ya
SMG moja na iliyo futwa namba na kukatwa kitako na mtutu,magazine moja
na risasi kumi katika upekuzi nyumbani kwake polisi wamefanikiwa kupata
vitu kadhaa vikiwemo simu mbili za mkononi , CD 21 za picha mbalimbali
deki moja,viatu pea mbili na tochi mbili na mpira wa baiskeli moja na
bidha mbalimbali za dukani.
Pia
Kamanda alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 1.45 Februari 7,
2014 katika Kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Mjini Musoma mkoani Mara
ambapo marehemu ameuawa kutokana na taarifa zilizo tolewa na Bw Charles
Chacha Kichune maafuru (kenonke) ambaye amemtaja marehemu kuwa ni
mshirika wake.
Kamugisha
ameshukuru jeshi la polisi Mkoa wa Tanga kwa kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi Tarime/Rorya kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa.Pia
amewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea kufanya shuguli zao kama
kawaida wakati hatua zingine zinachukuliwa .
Aidha
amewataka wananchi kutoa ushirikiano na yeyote atakaye toa taarifa ya
jambazi kukamatwa atapewa zawadi ya Tsh milioni moja papo hapo.
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA JUMATANO PATA KOPI YAKO"
No comments:
Post a Comment