Dr.Wilbroad Slaa, leo kaatika viwanja vya CC
ILOMBAJijini Mbeya, amesema licha ya mapokezi mazuri aliyooneshwa na
wafuasi wake, lakini hajafurahishwa na jeneza lililokuwa limetengenezwa
huku msalaba wake ukiwa na jina la mtu aliyehai Zitto Kabwe.
Amesema hali hiyo haipendezi kwasababu ishara ya jeneza inatisha hasa ikionesha taswira ya kumzika mtu aliye hai.
Alisema kumfukuza Zitto ni ishara ya chama chake kuthubutu kufanya yale watakayoyasimamia watakapoingia Ikulu ambapo yeyote atakayekiuka katika, atashughulikiwa na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wanaokiuka sheria za nchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu), alisema amepata taarifa za Chama Cha Mapinduzi(CCM), kuandaa kambi la vijana wa kuvuruga mikutano ya Chadema ambalo lipo katika shule ya Sekondari ya Chimala, inayomilikiwa na Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoani Mbeya.
Taarifa hiyo imepuuzwa na baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM, ambao wamesema kambi la vijana hao ni kwa ajili ya halaiki ya sikukuu ya miaka 37 ya CCM Taifa, sherehe zinazotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya na mgeni rasmi atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete.

"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA SIKU YA JUMATANO KWA SHILINGI 500 TU"
No comments:
Post a Comment