TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, October 25, 2013

WAREMBO 800 KURINDIMA NDANI YA CLUB MAISHA LEO, DVJ MAJEY, HYPERMAN NA ZUNGU MYAMA WAAHIDI BALAA KUBWA SHOW HAIJAWAHI TOKEA, BONGO MOVIE NAO KUFANYA VURUGU ZAO….. NI IJUMAA YA LEO!


Na Livingstone Mkoi
Leo ni leo waswahili wanasema asiyekuwa na mwana abebe stone itakuwa mzuka vilevile siku ya leo Jiji la Dar na vitongoji vyake vitatikisika kwa mshtuko wa burdani moja tu na ya kijanja inayotarajia kufanya usiku wa leo palepale kwenye kiota namba moko cha burudani Bongo CLUB MAISHA.
Mpango mzima wa show hii ya kijanja na kitemi ilipewa jina la BAVARIA BLACK 8.6 LAUNCH PARTY team ya LIVE DJ DRUMMER chini ya Zungu mnyama, DJV Majey pamoja na Hyperman Kizo mnyama watarajia kuwadatisha na staili hiyo mpya Tanzania ya upigani live wa disko.
Akitema cheche hizi the big bos wa kila done la burudani ndani ya Maisha Club Gila alisema “ Ninaweza kusema kuwa siku ya leo tarehe 25 Octoba Club nyingine zitasimamisha huduma kupisha show hii moja ya kijanja na kipekee na huenda haijawahi kufanyika kwenye ardh hii ya Kamanda Kova hivyo mashabiki wahakikishe wanatumia fursa hii vizuri kwani wasije kujutia baada kuhadithiwa” Alisema Gila
Aidha mpango mzima wa show hiyo namna ya kuzama ndani mashabiki watalazimika kuacha kile kinoti chekundu mlangoni kwenda kushuhudia gharika hiyo ya burudani.
Akiongea na Blog hii mwana drum Zungu Mnyama alisema kuwa leo hatokuwa na mchezo atacharaza drum kwa mtindo wa non stop ili kuwadatisha mashabiki wake. Bongo movie na warembo wazuri zaidi ya mia 800 watakuwepo ndani ya Club hiyo kula bata pamoja na kushuhudia party hiyo ya aina yake.

No comments:

Post a Comment