TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, August 20, 2013

BREAKING NEWS: MWINJUMA MUUMIN NA WAZIRI SONYO WATWANGANA MAKAONDE. MUUMINI APIGWA KUMI ZA CHEMBE NA KUSHINDWA KUPUMUA HALI NI MBAYA ENEO LA TUKIO. UNGANA NA XDEEJAYZ.BLOGSPOT.COM

 Aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Victoria kabla ya jana kupigwa chini kwenye bendi hiyo.
  Waziri Sonyo kushoto.
 Na Mwandishi Wetu
Habari zilizonaswa na mtambo wa blog ya xdeejayz hivi punde zinasema kuwa kumezuka ugomvi mkubwa sana kati ya aliyekuwa Rais wa bendi ya Victoria Muumini Mwinjuma na Waziri Sonyo kuzitwanga kavu kavu na kuumizana vibaya.

Chanzo cha xdeejayz kilichopo eneo la tuki huko Mbagala Magengeni kwenye ukumbi wa Bouble D zinasema hali si swali eneo la tukio " Yani nyie Xdeejayz mngefika hapa haraka mje kuchukuwa picha Muumini anapigana na Waziri Sonyo hali ni mbya sana kwani Muumini kapigwa sana ngumi za chembe zilizopelekea kushiondwa kupumu vizuri" Kilisema chanzo chetu

Xdeejayz iliendelea kuelezwa na chanzo hicho kuwa ugomvi huo ulianza baada ya Muumin kumtuhumu Waziri Sonyo kuwa ndiye aliyesabaisha yeye kupigwa chni kwenye nafasi ya urais na kuwa muimbaji wa kawaida tu.
Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa siku ya jana Muumnio alipigwa chini kwenye nafasi hiyo na nafasi yake kupatiwa mty mwingine aliyefahamika kwa jina la Hamisi hali iliamsha hasira kwa Muumini ambae leo hii alifika mapema kwenye ukumbi huo wanaofanyia mazoezi akiwa kwenye hali ya shari shari ambapo baadae Waziri Sonyo nae aliingia na mara baada ya kufika tu Muumin alimurukia teke la shingo Waziri Sonyo ambae alikwenda moja kwa moja chni ambapo baada ya kuamka Waziri Sonyo nae alimshindilia ngumi kama kumi za chembe Muumin ambae alishindwa kupumua na kudondoka chini.
Xdeejayz baada ya kupata hizo taarifa ilivuta waya moja kwa moja kupita simu ya mkononi ya Muumini ambapo simu hiyo iliita tu bila majibu.

No comments:

Post a Comment