TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, May 21, 2013

BABA MZAZI WA DULLY SYKES ANASWA NA BANGI!

 Baba mzazi wa mwanamuziki wa bongo flava nchini Dully Sykes, Mzee Sykes pichani kama inavyoonekana akiwa na madawa harafu ya kulevya aina ya bangi mkononi huku mbegu mbegu zikiwa zimedondoka chini.



Dully Sykes

Na Livingstone Mkoi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa bongo flava nchini Dully Sykes Mzee Sykes hivi karibuni alinaswa na kamera ya Xdeejayz akichambua bangi mikononi mwake kwa ajili ya kuitumia.

Tukio hilo la aina yake lilitokea maeneo ya Magomeni Mikumi nyumbani kwa msanii aliyefahamika kwa jina la Shebo, na kushuhudiwa na papalazi wetu ambae alifanikiwa kumpiga picha mzee huyo akiwa na bangi mkononi mwake.

Mzee huyo akiwa hana shaka yoyote aliendelea kuchambua bangi hiyo huku mbegu zake zikidondoka chini kama mshare unavyoonesha hapo pichani.

Hata hivyo mzee huyo alishindwa kuendelea na zoezi la kuitayarisha bangi hiyo kutokana na kumtilia wasi wasi mwandishi wetu akidhani ni afande hali ilimfanya kukosa amani muda wote hadi mwandishi wetu alipoondoka na yeye alipata wasahaa wa kuendelea kuiandaa bangi hiyo.

No comments:

Post a Comment