TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, January 28, 2013

TOUR YA TIMU YA DAR LEOPARD CLUB ILIVYOCHENGUA MKOANI IRINGA MWISHONI MWA JUMA!





Watoto washabiki wa mchezo wa rugby wakipiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Dar Laopard ya Jijini Dar iliyokuwa nchini Zambia na Mkoani Iringa.






 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Dar Leopard Club wakiwa katika picha pamoja siku ya Jumamosi Mkoani Iringa kwenye mashindano ya mchezo wa Rugby yaliyopewa jina la Southern Highland "Touch Rugby



 Mmoja wa wachezaji nyota wa timu hiyo ambae pia ni mwandishi wa blog hii Livingstone akiwa hoi uwanjani baada ya mchezo mkali.



 Ilikuwa ni misosi ya kitasha tu sio ugali au wali hapa ilikuwa Mabaga,Mapizza nk kama ilinayoonekana pichani.

 Hapa baada ya mechi ilikuwa ni kunywa maziwa mtindo mmoja kwani wadhani wa mashindano hayo ambao ni IRINGA ASAS DAIRIES walimwaga maziwa kama maji siku hiyo.

Hapa winga hatari wa timu hiyo akiwa ameuchapa usingizi baada ya safari ndefu pamoja na kula gambe za kutosha.

 PROP hatari wa timu ya Dar Leopard Livingstone Mkoi akiwa amepunzika kwenye Hotel ya kitalii waliyofikia wachezaji hao nje kidogo ya mji wa Iringa



 Hapa ni eneo la Mbuga za wanyama Mikumi kuna nyama za mbuzi za kumwaga pamoja nyama za wanyama poli timu ilishuka kwa ajili ya kula nyama.

 Hawamu Juma mwenye jezi ya misitari nyekundu na nyeusi akitafuna  nyama kwa hasina huku pembeni akiwa na mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.


 Mawinga hatari wa Dar Leopard kulia ni Hawamu Juma kushoto Jeremiah wakiwa wameuchapa usingizi ndani ya gari.Wakati timu hiyo ikitokea Zambia kuja Iringa

CAPTAIN wa timu ya Dar Leopard Geog Mtefu akijichagulia vipaja.Mbuzi hao ambao huuzwa kati ya shilingi elf kumi na elf nane.

Na Mwandishi Wetu 

Timu ya mchezo wa Rugby ya Dar Leopard ya Jijini imewasili leo asubuhi kwa ndege ya Flightlink ikitokea Mkoani Iringa kulikokuwa na mashindano ya Rugby kwa timu tofauti.

Akiongea na xdeejayz mmoja wa wachezaji wa timu hiyo Hawamu Juma alisema kuwa timu yao iliondoka Ijumaa iliyopita na kutua nchini Zambia na baadae kuja Mkoani Iringa kwa ajili ya kukamilisha ziara yao ya kimchezo.

Ambapo timu ambayo iliondoka ikiwa na wachezaji wote nyota ambao walionesha uwezo wa hali ya juu na kuwaduwaza wazungu ambao walishindwa kuamini kama wachezaji hao ni watanzani au laa.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano hayo ni pamoja Hawamu Juma, Livingstone Mkoi, Jeremial,Georg Mtefu, Erika Mura,Alfonce nk.

Kwa mujibu wa captein wa timu hiyo Georg alisema timu hiyo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa hivyo Ijumaa hii itaendelea na mazoezi makali kwenye uwanja wao wa nyumbani wa IST ya Masaki.

No comments:

Post a Comment