Super lady wa sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Yakiwa yamepita masaa kadhaa tangu Jiji la Dar kulipuka kwa habari za msanii wa filamu za kibongo Mainda kudaiwa kunasa ujauzito Xdeejayz imenasa taarifa mpya toka kwa mashabiki ambao wanadai kama kweli hizo taarifa za ujauzito zitakuwa za kweli basi mimba hiyo huenda ni ya Manaiki Sanga "the don".
Kwa mujibu wa watu wa karibu na wasanii hao walisema kuwa " Yani kama kweli Mainda kanasa kitu haki ya nani ni lazima itakuwa ya Manaiki Sanga kwani siku za hivi karibuni wamekuwa na ukaribu usio wa kawaida.
Hata hivyo mashiki hao wamefikia hatua ya kuwafikiria wawili kama wamepigana mimba kufuatia siku za hivi karibuni kuwa na ukaribu sana bila kutabainisha kama ni ukaribu wa kikazi ama jambo jingine.
Xdeejayz inafanya juhudi za kuwatafuta mastaa hao ili kuweka bayana tukio ili mashabiki zao wawe na amani lakini simu zao hazikupokelewa hadi tunarusha hewani taarifa hizi lakini tuna waahidi mashabiki wetu muda mwingine tutawaletea habari kamili.
CRDT: XDEEJAYZ
No comments:
Post a Comment