Maajabu yanazidi kuendelezwa chini ya Jua na watu wenye umaarufu na pesa
nyingi duniani wanaendelea kuonyesha jinsi wanavyoweza kutumia pesa za
kufanya maajabu ya Dunia.
Hayo anadhamiria kuyafanya Mwanasoka Maarufu, David Bekham ambapo yupo
kwenye mpango wa kujenga uwanja wa soka utakaokuwa ukitumiwa na timu
mpya inayomilikiwa naye.
Picha za muundo wa Uwanja huo zimetoka ambapo utakua ni uwanja unaoweza
kuingiza watu elfu ishirini na tano na unatarajiwa kujengwa katika eneo
la Port of Miami, Marekani.
Unaambiwa pia ndani ya uwanja huu wa kisasa kutakuwa mgahawa mkubwa pamoja klabu ya usiku.
Kingine ni kwamba uwanja huu ambao bado haujapewa jina utakuwa ukichezewa mechi 17 kwa msimu wa ligi kuu ya Marekani.
CRDT-XDEEJAYZ TANZANIA
No comments:
Post a Comment