Na Sakina Shabani
Miss Ruvuma
Isabela Mpanda” Mama Obam” Amekuwa mrembo pekee asiyechuja kimuonekano taofauti
na mamiss wengine ambao wamechoka na kugeuka mama wa nyumbani.
Watafiti wa
mambo ya uremo waliieleza Maskani Bongo kuwa Miss huyo kila siku siku
zinavyozidi kwenda anaonekana mtoto mdogo “ Kiukweli kwamba Isabela amekuwa
makini sana kuulinda mwili wake ona warembo wengine walivyochakaa utadhani
vikongwe na hii inatokana na mrembo huyo kuwa makini kwenye utumiani vyakula na
vipodozi ambayo mara nyingi huwaathiri warembo hao” Alisema Mama Situmai
Aidha
Mashabiki hao mrembo huyo ambae licha ya
sanaa pia ni mwana bongo flava
waliendelea kueleza kuwa tangu mrembo huyo atwae umiss Ruvuma ni miaka
sita na tayari amezaa watoto wawili lakini kimuonekana utadhani hajazaa kabisa.
Hata hivyo Xdeejayz ilimtafuta mrembo huyo ili kueleza siri ya mafanikio yake ambapo
alisema “ Kuna mambo mengi sana ya kufanya la kwanza ni kuepuka starehe za
kupindukia kama pombe kali, kukesha usiku kucha, kutakiwa kula mboga za majani
mara nyingi ndizo zinaofanya ngozi kuwa nyororo daima la mwisho ni mazoezi na
kutotumia vipodozi vyenye kemikali” Alisema Miss huyo
"NI WAKATI WAKO WA KUPATA VITU ADIMU KWENYE GAZETI LAKO PENDWA LA MASKANI BONGO KILA JUMATANO" ....XTREME DEEJAYZ WATAKUFA NA MTU KWENYE UZINDUZI WA CLUB MAISHA MORO
No comments:
Post a Comment