TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, July 5, 2013

UKATA WA MAISHA WASABABISHA Q JAY AOKOKE KANISANI, SASA HIVI ANAIMBA NYIMBO ZA DINI!

Q Jay
Na Livingstone Mkoi
Yule mwanamuziki aliyewahi kutamba sana kwenye kundi la "Wakali Kwanza" lililokuwa linaundwa na wanamuziki kama Joseline,Makamua pamoja na Qj mwenye picha hapo juu hivi karibuni aliamua kuyasalimsha maisha yake kwa Bwana Yesu ili kubadilisha mfumo wa maisha baada ya kuwa hali mbaya ya kuta.
Akiongea na kituo kimoja cha redio Jijini Dar Q Jay katika taarifa yake hiyo alisema kuwa ameamua kubadilsha maisha toka maisha ya kidunia hadi kumpokea Masihi ambapo hadia sasa ameshaiva kiimani ile mbaya hivyo ameamua kumutumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
Hata hivy Q Jay ambae miaka kadhaa iliyopita tangu ashuke kimziki alikuwa akiishi maisha ya magumu na ya kuunga unga kiasi cha kutia imani huku akijaribu kuchomelea mageti maeneo ya Kinondoni Moroco iliamradi pate ridhiki ya kupeleka kinywani.
Aidha katika Interview hiyo Q Jay aliwathibishia mashabiki wake kuwa ameokoka kiukweli kweli na sasa hivi kila anachokifanya anaongozwa na roho mtakatifu na bila kuambiwa kufanya hivyo hawezi kufanya kwa vile inakuwa ni mipango ya Ibirisi hivyo alimaliza kutoa uwito kwa mashabiki wake kuwa wakae mkao wa kula kuna mambo mazuri yanakuja soon

No comments:

Post a Comment