TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, July 5, 2013

IRENE UWOYA ACHORA TATTOO YENYE NYAYO NA JINA LA MWANAE KRISH.

 
Staa wa muvi za Bongo, Irene Pancras Uwoya ameonesha upendo wake kwa mwanaye Krrish Ndikumana kwa kujichora ‘tatuu’ mgongoni yenye nyayo (makanyagio) ya mtoto huyo na kuzisindikiza na jina lake kwa juu.

Baada ya mchoro huo kukamilika, Uwoya aliitumbukiza kwenye mtandao wake wa kijamiii wa Facebook na kutazamwa na watu kibao ambao waliipenda.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliozungumza kuhusiana na tatuu hiyo walisema Uwoya amefuata nyayo za wanawake wengi wa Kiafrika ambao wakishazaa huwapenda sana watoto kuliko baba zao.

“Picha ni nzuri, mama ameonesha upendo wake kwa mtoto lakini hii ni tabia ya wanawake wengi wa Kiafrika, wakishazaa mapenzi yote wanayahamishia kwa watoto badala ya waume zao.

“We fuatilia utagundua ndoa nyingi huanza kuyumba baada ya mke kujifungua, maana mapenzi yote yanahamia kwa mtoto, mume kama hana subira anaanza kutafuta mwanamke mwingine wa kumpenda upya.
“Inawezekana Uwoya mwilini mwake hana tatuu hata moja ya mumewe, lakini Krrish kamchora nyayo ili kuwaoneshea wadau wake,” alisema Oscar Samuel, mkazi wa Mwenge, Dar

No comments:

Post a Comment