Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq.
Mkuu wa Wiyala ya Kinondoni akiwa na wakazi hao wa Nakasangwe kata ya Wazo akiwasikiliza malalamiko yao juu ya mafisadi hao, na Dc huyo kugundua wazi kuwa kuna uonevu mkubwa kwa wakazi hao.
Wamtaka
afike kuona nguvu ya ufisadi inavyofanya kazi huku baadhi ya watumishi
wa Manispaa ya Kinondoni wakihusishwa. DC Makonda Apongezwa.
Na Mwandishi Wetu
Wakazi
wa Kata ya Wazo na
Nakasangwe wamemuomba Rais Dokta John Pombe Magufuli kuanza ziara kwenye
kata hiyo ili kushuhudia uonevu na ubabe unaofanywa na watu wanaojiita
wawekezaji kwa kuwavunjia watu makazi yao huku wakidai kuwa ni yao.
Wakazi
hao ambao wamesheherekea zaidi ya siku 3 ushindi wa Rais huyo ambae
wanamini ataweza kuwasaidia na kuwasambaratisha mafisadi hao ambao wana
nguvu ya ajabu kutokana na kuwa na pesa nyingi ambazo ilidaiwa waliweza
kuhonga baadhi ya watumishi wa Mkoa pamoja na Manispaa ili wawezeshe
kuwavunjia nyumba zao na kuwahamisha na zoezi hilo lililofanikiwa.
Katika kikao kilichofanyika hivi karibuni cha Mkuu
wa Wilaya aliandamana na Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni, Afisa
Ardhi wa Manspaa na maofisa wengine toka Wilayani akiwepo RPC Wambura na
kwa kauri yake Mkuu wa Wilaya hiyo na wakazi walioathirika na ubabe huo
wa wawekezaji, Dc huyo aligundua chanzo cha mgogoro huo kuwa ni rushwa
na si kitu kingine na kuahidi kupambana kwa kadri atakavyoweza ili
wananchi hao wapate haki yao ya makazi.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa angalizo kuwa mgogoro huo huenda nyuma
yake kuwa na mtu mwenye nguvu kuliko yeye hivyo ni heri pia wananchi
hao wakashirikiana na Mwenyekiti wao wa mtaa ili wapate timu itakayokuwa
inasimamia ufatiliaji.
Wakiongea
na gazeti hili wakazi wa eneo hilo ambao waliothiriwa na ubabe wa
mafisaidi hao mmoja wa wakazi hao ambae ni mwandishi wa kituo cha E-fm
Radio Bwana Livingstone Mkoi alisema" Kiukweli hali haikuwa nzuri tangu
2012-13 wananchi wengi tulipoteza mali zetu, makazi yetu mengi yavunjwa
kibabe na Polisi waliodai kutumwa na Mkuu wa Wilaya aliyepita Mh Jordan
Rugimbana kwa madai kuwa sisi tumevamia eneo la mwekezaji, na kila
tulipoenda ofisini kwake kwa ajiri kufanya mazungumzo ya amani na
kumueleza kama eneo hilo sisi tulipewa na Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa
Mh Yusuph Makamba, alitoa majibu kuwa huo utekelezaji ni maagizo toka
ofisi ya Mkuu wa Mkoa" Alisema Mwandishi huyo
Mwandishi
huyo aliongeza kusema kutokana na nguvu fedha utekelezaji wa kubomoa
nyumba hizo ulitimizwa chini ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa
ubabe mkubwa, lakini hata hivyo suala hilo lilitinga kwenye chombo cha
Sheria na hatimae wakazi hao walishinda kesi na Manispaa kuamuriwa
kuwalipa fidia wakazi hao kwa vile walikuwa wakiishi kihalali eneo hilo
kwa vile upande wa team mafisadi ulishindwa kuwakilisha vielelezo vya
msingi vinavyoonesha kuwa hilo ni eneo lao, hata hivyo katika hali
nyingine mafisadi hao walifungua tena kesi nyingine ambayo inaendelea
hadi sasa.
Hata
hivyo wakazi hao wanaimani na Rais Dokta John Pombe Magufuli atasaidia
kusambaratisha mtandao huo wa ufisadi ambao unaodaiwa kuanzaia ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Maofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinodoni ili wananchi hao
waishi kama watanzania halisi na kuondoa dhana kwamba wao ni wavamizi na sio raia wa Tanzania ndio kesi waliyopewa, huku tuhuma hizo zikiletwa kwenye kipindi kisichokuwa cha uchaguzi lakini kipindi cha uchaguzi madai hayo huwa hayapo.Credit: maskanibongotz
No comments:
Post a Comment