Norberth Edward Hizza na Brigitte Vitalis ambao wote imeelezwa wanaskwa kwa utapeli kwa dada huyo wa Kiarabu, na tayari picha zao zimeshasambazwa kwenye magazeti karibia yote nchini kwa ajiri ya kurahisha kukamatwa kwao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura ambae anfahamu hili suala toka mwaka na ndiye awar aliyefanikisha kukamatwa kwa Brigitte Vitalis kabla ya hivi karibuni kudaiwa kwenda kuwatapeli dada wa Kiarabu na Mwandishi wa Habari Teddy Dinghoka
Surutana Khamis ambae ndiye mwenye MA/RB/9768/2015 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU ambayo ameifungulia kituo cha Polisi Magomeni huku Mkuu wa kituo hicho akitangaza kiama kwa Dada huyo na mumewe kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingi kituoni hapo zinazomlipoti yeye.
Irene Kafanabo ambae ni Dada Norberth Edward Hizza aliyekuwepo nae kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu dhahama wanayoipta kwenye familia kutokana na matukio hayo ya utapeli yanayofanywa na wifi yake huku kakaake akiingizwa kwenye mkumbo.
Kila mmoja ana RB yake, aishi kama Digidigi, Mumewe aingia
mitini kwa aibu ya udhalilishwaji. Zawadi nono kutolewa kwa atakaefanikisha
kukamatwa kwake. MA/RB/9768/2015 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU,
OB/RB/11345/2014 JALADA LA UCHUNGUZI
Na Mwandishi Wetu
Katika hali ya kushtua mwanamke mmoja ambae ni mzaliwa wa
Mwananyamala lakini kwa sasa anaishi Mtoni Jijini Dar aliyefahamika kwa jina la Brigitte Vitalis amedaiwa kuwapiga wanawake
wenzake zaidi ya 50 kwa njia ya utapeli.
Wakizunngumza na waandishi wa habari kwenye Hotel ya Itumbi Jijini Dar wakina dada hao ambao kila mmoja alipigwa kwa staili yake walisema
kuwa walifahamiana na dada huyo kwenye magroup huku wengine walifahamiana toka
wakiwa watoto.
Wakina dada hao walianza kusema kuwa msichana huyo alimfata
mmoja wa wakina dada hao aliyefahamika kwa jina la Anna na kumwambia awatafute watu kuna kazi ya supermarketinafunguliwa maeneo ya Sinza hivyo.
Akiongea kwa masikitiko dada huyo aitwae Anna alisema “Kaka
kiukweli kutokana na watu wengi kukosa
ajira mara baada ya kupokea mchongo huo watu walichangamkia tenda haraka na
kufika nyumbani kwangu ili niwape maelekezo zaidi” Alisema Anna
Hata hivyo msichana huyo aliendelea kusema Brigitte alimwambia kuwa lakini ni lazima
watoe laki mbilimbili kwa hawa wafanyakazi wa kawaida lakini kwa anaehitaji
cheo cha umeneja au uongozi wowote basi atatoa kuanzia milioni moja, ndipo watu
haraka wakaanza kuingia mtaani kusaka pesa na kisha wakampatia Anna ambapo
zaidi ya milioni 9.
Msichana huyo aliongeza kusema kuwa mara baada ya kupata hizo
pesa alimpigia Brigitte na kumwambia pesa zipo tayari hivyo aje achukue na
alifika haraka na kuchukua mzigo huo wa maana kisha akawambia watafute siku
kisha awakutanishe na meneja wa supermarket hiyo ili awape maelekezo namna ya
kwenda kuanza kazi hiyo.
Hata hivyo baada ya siku hiyo kukutana na meneja kufika kweli
Brigitte alikuja na mvulana mmoja ambae anasili ya Kiasia ambae alivaa shati
yenye jina la hiyo Supermaketi, lakini hata hivyo walianza kushtuka baada ya kuona muhindi
aliyekuwa amekuja kushtuka kwa kuona uwingi wa watu na akamuita huyo Anna na
kumuuliza mbona watu wengi hivi wote hao wanataka kazi?.
Muhindi huyo alipojibiwa ndiyo na kuelezwa kama wote hao
wametoa pesa zao kwa ajiri ya ajira hali iliyomfanya muhindi huyo kupigwa na
butwaa kisha akawambia yeye hakupata
pesa yoyote hivyo wamalizane na Brigitte kwanza kwani hawezi kuwatafutia kazi
kundi lote la watu.
Hadi hapo watu wakagundua kama tayari amepigwa ndipo walienda
kufungua taarifa kwenye vituo mbalimbali vya Polisi, huku msichana ambae ni
mwarabu nae aitwae Surutana Khamis nae akipigwa milioni tisa dukani kwake
baada ya Brigitte na mumewe aliyefahamika kwa jina la Norberth Edward Hizza
kudaiwa kwenda kuchukua tv2, pamoja na simu 3 za
gharama.
Hata hivyo baada ya matukio hayo wakina dada hao wali kwa
nyakati tofauti walifungua taarifa kwenye vituo vya polisi vifuatavyo, MA/RB/9768/2015
KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU, OB/RB/11345/2014 JALADA LA UCHUNGUZI na
baada ya hapo wakina dada hao walifika kwa RP wa Kinondoni kwa ajiri ya msaada
ndipo Brigitte alipokamatwa kisha kufunguliwa mashtaka, huku kesi ikiwa
inaendelea kwenye mamlaka husika alimpiga tena dada mmoja mwandishi wa Habari
aliyefahamika kwa jina la Teddy Dinghoka milioni kumi na mbali.
Habari zaidi toka kwa wakina dada hao zilisema kuwa Brigitte
amekuwa akijitambulisha kama yeye ni mfanyakazi wa Un au taasisi za Serikali za
Bank huku akiwa na sare za bank moja maarufu.
Hata hivyo licha ya msaada mkubwa waliopatiwa na Kamanda
Wambura wa kumkamata mtuhumiwa huyo na kukubar kuwalipa watu hao lakini
hakufanya hivyo hadi leo na huku akiendelea kuwapiga watu wengine na sasa
anaishi kama digi digi kwa kuhofia mkono wa dola kwani tayari safari hii akikamatwa
moja kwa moja mahakamani kisha kwenda jela.
Baada ya taarifa hizo walitafutwa Brigitte na mumewe Norberth
Edward Hizza ili wazungumzie tuhuma hizo na Brigitte ndiye aliyepatikana na
kushindwa kutoa ushirikiano kwa kusema yupo bafuni anaoga na atapiga baadae
lakini kila alipopigiwa hakupokea tena simu hadi gazeti hili linakwenda
mitamboni.
Wakina dada hao wameahidi zawadi nono kwa mtu atakaefanikisha
kukamatwa kwa mdada huyo au mumewe, kwa sasa Brigitte amekimbia kwa mumewe na anadaiwa
kukimbilia kwa mamaake Tegeta.
Wadai hao wametoa uwito kwa wananchi mbalimbali watakao waona watu hao wawasiliane na kituo chochote cha Polisi au wachukue kumbukumbu hizi
MA/RB/9768/2015 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU, OB/RB/11345/2014 JALADA LA UCHUNGUZ na wao wapo tayari kutoa zawadi nono kwa watakofanisha sula hili ambalo ni la kweli na Jeshi la Polisi wanafahamu.
MA/RB/9768/2015 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU, OB/RB/11345/2014 JALADA LA UCHUNGUZ na wao wapo tayari kutoa zawadi nono kwa watakofanisha sula hili ambalo ni la kweli na Jeshi la Polisi wanafahamu.
Credit:maskanibongotz
No comments:
Post a Comment