TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, May 9, 2014

SIKU 40 ZA MAAJAABU YA 93.7 E-FM, WASIKILIZAJI ZAIDI YA MILIONI 10 WAMEITEGEA SIKIO KWA MUDA HUO MCHACHE ANGALIA KINACHOENDELEA SASA..!



Na Livingstone Mkoi
Toka ianze kusikika rasmi kwa watanzania ilikuwa tarehe 2/4/2014 Radio mpya inayopatikana masafa ya 93.7 E-FM imeonesha nguvu ya ajabu tofauti na radio nyingine mpya zinapokuwa zinaanza kusikika.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa mtandao huu umeonesha kituo hicho kipya cha burudani za nyanja zote bila ubaguzi wala itikati kwa kipindi kifupi tu imetikisa nchi kwa kusikilizwa na watu wengi zaidi na kuvunja rekodi ya kipekee.
93.7 E-fm inapatikana jiji ni Dar na tayari  imebamba ile mbaya kila sehemu watu wanasikiliza radio hiyo ambayo ndani yake kuna vionjo vya aina yake ambavyo kamwe huwezi kuvipata sehemu nyingine yoyote kwani hali iliyopelekea watu wengi kuipenda huku wakiriwadhika na burudani za aina zote.
Hata hivyo cha kuvutia pindi usikilizapo radio hiyo ni namana ambavyo inaweza kukufikisha nyumbani kwako huko kijijini kwa kusikiliza nyimbo za makabira ya nyumbani hali ilitopelekea watu wengi kukumbuka kwao kwa kuitegea radio hiyo ya vijana.
Taarifa za ndani toka chanzo chetu kilichopo ndani kituo hicho kinasema kuwa uzinduzi wa kutikisa nchi unakuja hivi karibuni wenye lengo la kuwakabidhi wasikilizaji radio hiyo pamoja na kupata baraka zao.

No comments:

Post a Comment