KUMBE UGOMVI WA WOLPER NA UWOYA CHANZO KILIKUWA KUGOMBANIA PEDESHEE, LAKINI SASA WAUNGANA KUWA KITU KIMOJA ANGALIA HAPA...!
Irene Uwoya na Jackline Wolper
Ule uhasimu uliokuwepo kwa takribani miaka miwili sasa kati ya mastaa
wakubwa na warembo Swahiliwood Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye
umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi. Wawili hao walidaiwa kuingia
katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media
ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema
kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu
kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper. Hata hivyo habari nyingine zilizoifikia Xdeejayz mapema leo zinasema kuwa kumbe ugomvi huo chanzo ilikuwa ni kumgombea pedeshee mmoja mwenye pesa chafu.
No comments:
Post a Comment