Marehemu Mangwair enzi za uhai wake.
Mfano wa jengo la Night Club ambalo inadaiwa angejenga mwanamuziki Mangwair maeneo ya Kihonda Mkoani Moro.
Kwa ndani ingeonekana kama hivi Club hiyo.
Huenda ingekuwa Club ya kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kati.
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Habari nyeti toka ndani ya familia ya Arbeth Mangwair zimesema kumbe mwanamuziki huyo alikuwa na ndoto ya kufungua Night Club kubwa maeneo ya nyumbani kwao huko Mkoani Morogoro.
Akiongea na Xdeejayz kwa sharti la kutotajwa jina kwa maana yeye si msemaji wa familia mtu huyo alisema " Ndugu yetu alikuwa na mikakati ya kujenga Night Club kubwa sana hapa hapa maeneo ya nyumbani kwenye uwanja wa babaake na tayari familia ilikuwa imeshampa baraka zote" Alisema msichana huyo ambae ni ukoo mmoja na Ngwair
Aidha Bint huyo aliendelea kumueleza mwandishi wetu kuwa hata huko nchini Afrika Kusini alikuwa kwenye utafiti wa kuangalia namna jengo hilo litakavyokuwa huku akitafuta wadhamini wa kumsaidia jengo hilo ambalo lingekuwa na thamani ya mamilioni ya shilingi.
Hata hivyo msichana huyo alishindwa kufafanua kama familia hiyo itaweza kuendeleza mipango ya marehemu au kama kuna mwana familia yeyote aliyechaguliwa kusimamia plans hizo.
No comments:
Post a Comment