Mapema leo wakazi hawa wakiwa Nakalekwa CCM wakimsubiri Mh Paul Makonda
Mabango yaliyokuwa yanampongeza Dc Makonda kwa kujito muhanga kupambana na mafisadi ili kuwatete wananchi hao wanyonge
Dc akiingia eneo la uwanja wa Nakalekwa kwa ajiri ya kuzungumza na wakazi hao tayari kwa ajiri ya kuanza zoezi la kuhakiki viwanja vyao ili baadae wapimiwe na kumaliza mgogoro huo ulimshinda Dc aliyemtangulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni wa sasa.
Mh Makonda akipokelewa na mabango kama hivi
Mh Makonda akishangaa mabango mbalimbali yaliyokuwa na ujumbe tofauti kama yanvyoonekana
Moja ya bango linasomeka hatumtaki DASI ambae ni msaidizi wa DC Makonda ambae anatuhumiwa kushirikiana na mafisadi hao kuhujumu wananachi,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo hii bila hekima na kauri nzuri za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda kwa wakazi wa Nakasangwe na Nakalekwa waliopo kata ya Wazo wenye mgogoro wa ardhi basi huenda tungeripot tofauti habari kutokana na ghazabu kubwa waliyokuwa nayo wananchi ya kuwakataa watu wa mipango miji, Maafisa Ardhi, na Msaidizi wa Mkuu wa Wailya Mheshimwa Dasi wasishiriki zoezi la kuhakiki viwanja vyao.
Mwandishi wa Maskanibongotz aliyekuwepo eneo la tukio amesema kuwa hali ilikuwa mbaya baada ya wakazi hao kuibuka na mabango yenye kumuomba Rais Magufuli amuongezee nguvu Paul Makonda kwa vile kwenye zoezi hilo ni kama yupo peke yake kwani karibia watumishi wote walitajwa kudaiwa kuhusika na rushwa toka kwa mafisadi hao.
Wakizungumza na maskanibongotz watu hao walisema " Jamani Makonda amejitoa muhanga lakini hana sapoti hivyo kupitia nyie waandishai wa habari tunaomba mfikishie ujumbe wetu Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa tunamuombsa amuongezee nguvu Makonda kwani hapa amezungukwa na wasaliti watupu sisi tunajua kinachoendelea" Walisema watu
Aidha watu hao walisema hata jana kitendo cha maafisa Ardhi hao kuchelewa kulikuwa na namna ambapo indaiwa walikuwa na kikao kingine na mafisadi hao na kuna taarifa kuwa pia kuna nyaraka za ardhi wameshawatengezea mafisadi hao ili kuwakandamiza wao.
Baada ya Mkuu huyo wa Wailaya kuona jazba za wakazi hao alilazimika kutumia maneno yenye hekima na busara pamoja na kuwaomba wakazi hao wasijari yeye mwenyewe yupo na atashiriki siku mbili kisha atawaacha watumishi hao waendelee na pia wakazi hao wawaamini watumishi wake.
Wakazi hao walikubari kwa shingo upande lakini bado walizidi kumuomba Mh Rais amuongezee nguvu Makonda kwa vile kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kutokana na kuzngukwa na wasaliti kwa madai hayo ya kuwabeba mafisaidi wanaotaka kuchukua eneo kubwa hukuwakazi hao elfu mbili na mia tano waachwe bila makazi jambo ambalo hata kwa Mungu halina baraka.
Aidha wakazi hao wamempinga Mhe Makonda kuwaacha watumishi hao peke yao kusimamia zoezi hilo kwani tayari wanatuhuma za kushirikiana na mafisadi, huku wakisisitiza Rais Magufuli amuongezee nguvu.
Hata hivyo kwa madai hayo ya wakazi hao kuwatuhumu watu nwa ardhi, Mipango Miji na Msaidizi wa Makonda kuwa watuhumiwa kwa ufisaidi wananchi mbalimbali wapenda amani wamemuomba Rais kupitia ujumbe wa wananchi kufanya uchunguzi wake kama alivyoahidi siku alipolihutubia bunge Dodoma kuwa kwa mtumishi yeyote atakaebainika kwa ufisaidi ama rushwa na ushahidi ukiwa sawa basi watimuliwe hivyo basi angeanza kwa maafisa hao.
Credit: maskaningotz
No comments:
Post a Comment