TANGAZO MAALUM
TANGAZA NA SISI
Tuesday, June 24, 2014
Goodnews Kwa mara ya kwanza ndege ya @fastjet yarushwa na maarubani Watanzania.
Jina la fastjet sio geni Tanzania na hii ni kutokana na kuzidi kukua kila siku kutokana na huduma inayotolewa kusafirisha abiria kutoka kona kadhaa za Tanzania kwa kuzingatia muda na bei nafuu pia.
Good news ni kwamba shirika hili la ndege ambalo limekua likisafirisha abiria wa ndani ya nchi kati ya Dar es salaam na Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro kwa sasa, limeanza kuwapa shavu marubani Watanzania.
Kwa mara ya kwanza Marubani Watanzania Arif Jinah na William Zelothe wameirusha ndege ya abiria ya Fastjet A319 mpaka Mwanza wakiwa wamezingatia viwango vya usafirishaji vya kimataifa ambapo marubani hawa wako kwenye idadi ya Marubani zaidi ya kumi Watanzania walioajiriwa na fastjet.
Siku zote wafanyakazi ndani ya ndege na kwenye ofisi zao ni Watanzania kwa asilimia kubwa ila Marubani ndio hawakuwa Watanzania.
Unaambiwa fastjet ilipoanza kufanya kazi Tanzania ilikosa marubani wanaoweza kuendesha ndege aina ya Airbus na ndio maana hii ni good news manake Watanzania wa kwanza wameweza kufuzu na kuendesha ndege wao wenyewe.
Hongera sana kwa rubani Arif Jinah na William Zelothe.
Kwenye sentensi nyingine nimeona nikuachie na hii good news nyingine ya Fastjet kuanza kusafirisha abiria kati ya Dar es salaam mpaka Harare August 5 2014 ambapo wataanzia kwa safari mbili kwa wiki.
Safari ya fastjet kati ya Zimbabwe na Tanzania inakua ya tatu kimataifa huku nyingine zikiwa ni kati ya Dar es salaam na Johanesburg South Africa pamoja na safari ya Lusaka Zambia huku zikiwa ni safari za bei ndogo kabisa pale abiria anapowahi kufanya booking.
Unawazungumziaje fastjet mtu wangu? umeonaje shavu walilowapa Watanzania?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment