MISS Kiswahili 2008 Bongo, Rehema Fabian amenagwa vibaya na wadau baada kutupia picha za utupu katika mtandao wa
Instagram.
Shabiki mwingine aliyeona picha hizo mtandaoni, alichangia kwa kusema staa huyo hana lolote la maana analolifanya tangu atwae taji la u-miss zaidi ya kuweka picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.
“We kila siku habari zako ndiyo hizohizo, kwa nini usitafute kazi nyingine ya kufanya na kukuingizia kipato?” ilisomeka komenti hiyo katika mtandao wa Instagram.
Baada ya kupata malalamiko hayo ya kumponda Rehema kutoka kwa mashabiki tofauti, paparazi wetu alimcheki nyota huyo kupitia simu yake ya mkononi, alipopatikana alifunguka:
“Nimepiga mwenyewe na kuziweka katika ukurasa wangu, sasa nashangaa hao wanaosema eti najidhalilisha kwa lipi hasa?
"SIKU ZINAHESABIKA KABLA YA 93.7 KUWAFIKIA WANANCHI ENDELEA KUFATILIA HABARI HII NJEMA KWA MSHABIKI WA BURUDANI TANZANIA KUPITIA BLOG HII NA GAZETI LA MASKANI BONGO"
No comments:
Post a Comment