TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, March 28, 2014

WAISLAM KUMTENGA DIAMOND KISA UPUUZI HUU ANGALIA HAPA ALICHOKIFANYA KINASHANGAZA..!


Kijogoo wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz akicheza staili ya Ngololo kwenye kaswida.



KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.

Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.

Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.

Diamond akiwa kwenye shughuli hiyo.
“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.

Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.

...Diamond akiwa na mtoto wa Moze Lyobo aliyefanyiwa Maulidi.
“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.

No comments:

Post a Comment