TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, March 27, 2014

ANGALIA PICHA ZA RAIS UHURU KENYATA ALIVYOSIMAMISHA GARI NA KULUA CHAKULA KWA MAMA NTILIE NA KUNYWA MAJI YA KANDORO HII HAIJAWAHI TOKE KWA MARAIS EAST AFRIKA. XDEEJAYZ LIVE..!



Vituko vya mara kwa mara haviishi kwa Raisi wa Kenya, Bwana Uhuru Kenyata, ambapo wiki hii wakati alipotoka kwenye mkutano wake yeye na marais wengine aliamua kusimamisha msafara wake na kupata chakula cha mchana eneo la kawaida kabisa.
Tukio hilo limewashangaza wengi ambao walikuwa wakishangaa msafara huo wa Rais ukipita mara ghafla ukakata kona na kupaki pembeni na waheshimiwa kushuka kupata mlo wao wa mchana kwenye eneo liitwalo Kaijado tena chini ya mti.
Walioshuka kupata chakula cha mchana ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto pamoja na wasaidizi wao.

Rais Kenyatta anaonekana kuwa karibu na kutaka kuishi maisha ya kawaida tofauti na yale ya waheshimiwa maraisi wa nchi zingine, ambapo wiki iliyopita video moja ilimuonyesha akinunua karanga kwa muuzaji anayetembeza mtaani.
Hakuishia hapo pia aliwahi kutembea jijini Nairobi bila msafara kama ilivyozoeleka hadi Trafiki akamshangaa aliporuhusu gari za upande huo na kumuona akiwa anaendesha gari hizo ambazo alizisimamisha kwa muda kidogo.

No comments:

Post a Comment