TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, December 17, 2013

UZINDUZI WA CLUB MAISHA MOROGORO WIKII HII, MBUNGE ABOOD NA RPC SHINOGILE NDANI!


Na Sakina Shabani Morogoro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shinogile na Mbunge wa Morogoro Mh Abood wanatarajiwa kuwa moja ya  wageni rasmi watakaoalikwa kuhudhuria uzinduzi tawi la Club Maisha Mkoani humo.
Akiongea na Xdeejayz Meneja wa Club hiyo Robert Frank alisema " Tumewaalika waheshimiwa hao kwa ajili ya kuja kufurahi na sisi wananchi wao kwani tarehe 19 ni utambulisho tu na tarehe 20 ni Uzinduzi rasmi hivyo tunaomba wananchi mji wa Morogoro na vitongoji vyake wafike kwa win gi kujionea maajabu ya Club Maisha na burudani inayotolewa" Alisema Robert
Aidha Meneja huyo aliogeza kusema kuwa sasa kila kitu kimekamilika hivyo wakazi hao wakae mkao wa kula na hii itakuwa historia kwa Mkoa huo kuwa na Club namba moja ambayo haijawahi tokea tangu kuanzishwa kwa mkoa huo

Meneja huyo alimaliza kusema kuwa wamefanya makusudi za dhati kuwaalika wakuu hao kwa vile ni viongozi pekee ambao ni vipenzi wa vijana wengi hivyo si vibaya wakakutana pamoja na kufurahi.
M" KWA HABARI ZAIDI KUHUSU CLUB HIYO NA RATIBA NZIMA YA BURUDANI ZINAZOTOLEWA USIKOSE KUSOMA GAZETI LA MASKANI BONGO"

1 comment: